Baadhi ya watu ambao wemeisha fika Wengine bado wako nje wanajiandikisha, bila shaka na wengine wako njiani wanakuja.
M2S kwa kushirikiana na Blog Pacha za Jamiiblog na Community pamoja na Jamiiforum tunawaleteeni Uzinduzi wa wa Kanda ya Dar es salaam unaofanyika Ubungo Plaza katika Hotel ya Blue Pearl Jijini Dar es Salaam. Tupo hapa kuwaletea live updates. Kwa wale wanaoweza kufika karibuni sana.
Watu wa Dar es salaam wameweka utaratibu wa kila mshiriki kuchangia Tsh 5000 na 10,000 kwa kila mshiriki kama gharama za kutunisha mfuko wao wa Kanda.
Mgeni rasmi ni Mwenyekiti Taifa Mh. Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr. Wilbrod Slaa.
Wageni wengine maalum ni Wabunge wa Dar es salaam na Wajumbe wa Kamati Kuu waliopo Dar es salaam. Mpaka sasa namuona Mh. Mabere Marando.
=============
UPDATES
=============
Mh. John Mnyika ndio amemaliza kutoa salamu zake. Sasa anazungumza Henry Kileo katibu wa muda wa Kanda. anatoa mrejesho wa tokea Baraza Kuu nini kimefanyika hadi leo katika mchakato wa uundaji wa Kanda hii
Hery Kileo ndio amemaliza nae kutoa taarifa nzima ya mchakato wa uundwaji wa Kanda hii. Sasa ni Halima Mdee ambae alikuwa M/kiti wa Kamati ya uteuzi wa viongozi wa Kanda. Anatangaza uteuzi ulivyokwenda.
Sasa anaongea M/kiti wa Chama Mkoa wa Pwani Mh. Said Ukwezi yeye anatoa taarifa ya Maandalizi ya Mkutano wa hadhara wa kesho utakaofanyika Kibaha Mjini. Anasema maandalizi ni mazuri na watarusha njiwa wawili weupe kuashiria kazi ya M4C imeanza rasmi. anawakaribisha wadau wote Kibaha kesho. Anapigiwa makofi mengi na wajumbe
Sasa anaongea Mtafiti na Mwanamikakati wa Chama juu ya nini hasa kinatarajiwa katika Kanda hii ya DSM pamoja na wajibu walionao wanaKanda baada ya utafiti kufanyika. Amepewa dakika 15 mpaka 20. Anasema operesheni katika kanda hii itafanyika kwa njia ya mitandao, aridhini na hata angani. ambapo watapita mtaa kwa mtaa, mtu kwa mtu. Anasema changamoto kubwa ni fedha na rasilimali watu. anasema kutafanyika M4C fundraising ambayo itamhusisha kila mtu. Anasema suala la katiba ndio itakuwa agenda kuu katika mwaka huu na mwakani.
Dr. Slaa anawasalimu wananchi hapa ili amkaribishe M/kiti. Slaa anasema Magaidi jana wameonekana Bungeni. Anasema CHADEMA wako Makini kuliko serikali ya CCM, kuliko Usalama wa Taifa, Kuliko CCM wenyewe na umakini huo ndio utakaoiingiza CHADEMA madarakani. Anasema Serikali ndio inafadhili ugaidi na ndio magaidi wenyewe na kama si hivyo wasingempeleka Ofisa wake chumba namba 334 kumhonga ili atengeneze ushahidi wa kesi ya Lwakatare. Anasema wanazo taarifa zote muhimu kuhusu mambo serikali inayopanga dhidi ya CHADEMA. Amemkaribisha M/kiti Taifa nae ndio anatoa hotuba yake!
Mbowe anaanza kwa kutoa salam toka Bungeni. Anasema CHADEMA sio mpango wa Mbowe, wala wa Slaa bali ni mpango wa Mungu. Anasema Serikali inateka Mchakato wa Katiba lakini wakumbuke CHADEMA haina bunduki lakini ina watu. Anasema mpaka April 30 kama serikali haitaleta taarifa muhimu Bungeni juu ya mchakato wa Katiba CHADEMA itajitoa katika mchakato huo na itamwambia Prof. Baregu arudishe gari, nyumba na ajitoe.
Anasema walianza na Propaganda za Chama cha Mbowe, mara cha Wachaga, mara cha Kaskazini, mara cha Wakristo sasa wanadai cha Magaidi. Mbowe anasema hawezi kupoteza muda wake kumzungumzia mtu kama Mwigulu Nchemba atampandisha sana chati. Anaomba asimzungumzie mtu kama Mwigulu
Mbowe anasema udini katika nchi hii umeanzishwa na Kikwete wala hakuna haja ya kumumunya maneno. Anasema wana majina ya vikundi vilivyofadhiliwa na Ikulu kuzunguka nchi nzima kueneza sumu hii ya udini. Anasema muda si mrefu watawataja kwa majina kama watalazimishwa kufika hapo.
Anasema Pinda hafai kuendelea kuwa Waziri Mkuu kwa sababu anaunda tume kuchunguza tatizo la kufeli wakati tayari ana ripoti ya tume kama hiyo iliyoundwa mwaka jana na hajaifanyia kazi. Anasema CHADEMA imejenga historia leo kwa watu kuingia kwenye mkutano wa Chama cha siasa kwa kulipia kiingilio cha Tsh 5000 na 10,000 na kujigharamia chakula. Anasema Viongozi wasizue wanachama wapya na anawapongeza Marando na Safari kwa kukubali kuiongoza Kanda ya Dar es salaam. Anasema Kanda zimeundwa kuwapa wanachama wengi zaidi fursa ya kuongoza na kwamba uongozi wa Chama sio Mbowe na Slaa tu bali kila Mwanachama anaweza kupewa fursa na akaiongoza vizuri
PICHA MBALIMBALIA KUONYESHA MATUKIO KATIKA PICHA KAMA YALIVYOTOKEA PICHA ZOTE KWA MSAADA WA BLOG PACHA ZA community blog na jamiiblog KWA HISANI YA jamiiforum.
Mijadala ya hapa na pale kabla ya kuanza mapema asubuhi
0 maoni:
Post a Comment