Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA KUWA MGENI RASMI MORINGE SOKOINE MEMORIAL RUN ,MONDULI ARUSHA

Mbunge wa Monduli, Mh Edward Lowassa, anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika mbio za Sokoine Marathon, zinatakazofanyika Aprili 12, mwaka huu, wilayani Monduli, mkoani Arusha.

Mbio hizo zitafanyika katika kijiji alichozaliwa na kuzikwa  waziri mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine, ikiwa ni siku ambayo taifa litaadhimisha kumbukumbu ya kifo cha kiongozi huyo mkuu katika historia ya taifa la Tanzania.

Akithibitisha hilo Mratibu wa mbio za Sokoine Marathon 2013, Bw. Wilhelm Gidabuday alisema kuwa tayari wameshapata uthibitisha wa kuwepo kwa kiongozi huyo akiongozana na viongozi wengine wakuu wa nchi wakiwemo Mawaziri na Wabunge.

“Kutokana na wadhifa na heshima aliyokuwa nayo Marehemu Sokoine tumeona ni vizuri kuwaalika viongozi wetu wakuu wa nchi,na watu wengi tu watakuwepo, wabunge, mawaziri wakiongozwa na mheshimiwa Lowassa, wananchi wa kada mbalimbali, lengo ni kumpa heshima inayostahili kiongozi wetu,” alisema Gidabuday.

Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya maandalizi aliyepewa jukumu la kuwasiliana na viongozi ikiwa ni pamoja na Mgeni Rasmi, Mbunge wa viti maalum jimbo la monduli (CCM), Namelok Sokoine alisema kuwa, tayari wameshapata uhakika wa uwepo wa Lowassa katika mbio hizo.

Tulikuwa tunatarajia kumpata kiongozi wetu wa nchi katika Mbio za Sokoine Marathon,ila haitawezekana tena. Mbio hizo zitakuwa ni za kwanza kufanyika katika historia ya nchi hii katika maadhimisho ya kumbu kumbu ya kifo cha kiongozi wa ngazi za juu wa taifa letu, zinatarajiwa kushirikisha wakimbiaji zaidi ya 500 ambapo mpaka sasa tayari wanariadha 300 wameshathibitisha kushiriki.

Akizungumzia swala la kutoa namba pamoja na usajili, Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Arusha (ARAA), Joseph Jorwa alisema tayari utaratibu wa kuandaa namba umeshakamilika na kuongeza kuwa zoezi la usajili utafanyika baada ya siku kuu za Pasaka, katika Ofisi za ARAA, zilizoko katika uwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kwa ada ya sh. 2000 za Tanzania.

Sokoine Marathon zitahusisha mbio za kilometa 10 na kilometa 2 kutembea na kukimbia na zitatanguliwa na misa maalum zitakazofanyika katika kanisa la katoliki alililokuwa ni muumini kijijini kwake na zinatarajia kukutanisha watu mbalimbali kumuombea kiongozi huyo.

Taarifa hii imekujia kwa hisani ya Taifa Letu.Com kupitia Wazalendo25 Blog

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO