Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

NDEGE YA MAREHEMU MAWALA YAANGUKA ARUSHA NA KUUA RUBANI WAKE

Ndege ndogo iliyokuwa inamilikiwa na Wakili maarufu Marehemu Nyaga Mawala aliyefariki wiki 3 zilizopita na kuzikwa Jijini Nairobi, nchini Kenya imeanguka ikiwa katika hatua za mwisho za kutua (final approach) katika kiwanja cha ndege cha Arusha.

Taarifa zinasema kuwa ndege hiyo ilikuwa na rubani peke yake anayejulikana kwa jina la Jamal B S, au maarufu kama Bob Sambeke aliyekuwa anatokea West Kilimanjaro.

Maelezo zaidi kuhusu ajali hiyo ni kwamba ndege hiyo ilijaribu kutua baada ya masaa ya kawaida ya kufunga kiwanja(saa 12.30 jioni) kupita.

Taarifa za baadae zikaeleza kuwa aliyekuwa rubani “Bob Sambeke” amefariki dunia.
NDEGE ARUSHA

Huu ndiyo mti unao sadikiwa kugongwa na ndege kabla ya kupata ajari

Huu ndiyo mti unao sadikiwa kugongwa na ndege kabla ya kupata ajari

NDEGE ARUSHA 02

NDEGE ARUSHA 03

IMG-20130414-WA0002 copyMarehemu, Bob Sambeke ambae alikuwa rubani kwenye ndege hiyo iliyopata ajali

Chanzo: Jamii Blog (Pamela Mollel)

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO