katibu mkuu wa Chadema Dr. Slaa akihutubia umati mkubwa wa wananchi wa jimbo la Iringa mjini katika uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa leo
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini akiwapungia mkono wananchi waliojipanga barabarani kuwapongea wabunge wa Chadema na katibu mkuu wa Chama hicho leo
Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi akiwahutubia wananchi jimbo la Iringa mjini
Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akiwahutubia wakazi wa jimbo la Iringa mjini leo
mbunge wa jimbo la Ilemela mkoani Mwanza , Highness Kiwia
umati mkubwa wa wananchi waliofika kusikiliza mkutano wa Chadema Leo Iringa mjini
katibu mkuu wa Chadema Dkt Slaa (kushoto) akiwa na mbunge wa jimbo la Ubungo Jonh Mnyika katika mkutano wa wabunge wa chadema waliofukuzwa bungeni leo katika uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa
.............................................................................................
KATIBU mkuu wa chadema cha Demokrasia na maendeleo (Chadema ) Dkt Wilbrood Slaa amewataka wabunge wa Chadema kuendeleza ukali zaidi na wasiogope kufukuzwa na spika makinda .
Pia Dkt Slaa alisema kuwa ushindi wa Godbless Lema ni ushindi wa Mungu na kuwa wao kama Chadema walianza na Mungu na watamaliza na Mungu na kuwa hawata ogopa kamwa mabomu ya polisi kwani wao wanapigania ukombozi wa watanzania wote na sio Chadema.
Dkt Slaa ametoa kauli hiyo leo wakati akiuhutubia umati mkubwa wa wananchi wa mkoa wa Iringa katika uwanja wa Mwembetogwa jimbo la Iringa mjini.
Hivyo alisem,a kuwa kamwe hawatarudi nyuma katika kupigania maslahi ya taifa na kuwataka wale wanaokwenda kinyume na kusifia ufisadi lazima kuingiza Ikulu Chadema ili kulikomboa Taifa.
“Tulisimama Mwana yanga na kuwataja mafisadi 11 akiwemo Rais Jakaya Kikwete ila hadi leo hakuna kiongozi aliyesimama na kupambana na mafisadi hao .
Dkt Slaa alisema kuwa hana ugomvi na askari polisi ila ana ugomvi na viongozi wao na kuwa iwapo askari watatumwa kumpiga bomu basi wampige bila kuogopa kwa kuwa wametuma na mioyo yao inawaona.
Alisema kuwa CCM imeendelea kuifanyanga katiba ya Taifa hili na kufanya mambo ambayo wanayajua wao na kuacha kuwatumikia Watanzania na hivyo kuwataka askari polisi na wananchi wanyonge kuungana na Chadema katika kulipigania Taifa la Tanzania ili lisiendelee kuwa Taifa la mafisadi wachache wa CCM.
Alisema kuwa wapo ambao wanaeneza propaganda mbaya dhidi ya Chadema ila ukweli Chadema ipo kwa ajili ya kumkomboa mwananchi na hivyo kuwataka watanzania kuendelea kukipa nafasi Chadema ili kuipokea CCM Ikulu kutokana na CCM kushindwa kuwatumikia wananchi wake.
Alisema kuwa usalama wa Taifa upo kwa ajili ya CCM na ndio maana wanaendelea kukitetea chama cha mapinduzi CCM badala ya kuwapigania watanzania wanyonge .
Dkt Slaa alisema kuwa pamoja na usalama wa Taifa kujifanya wanajua kila jambo ila wengi wao hawajui katiba ya jumhuri ya Muungano wa Tanzania na ndio sababu wamekuwa wakifanya mambo bila kujitambua pamoja na wabunge wa CCM ambao wanakwenda bungeni kwa ajili ya kupongeza CCM bila kuwatetea wananchi .
Katibu mkuu huyo aliwashangaa wabunge wa CCM ambao siku zote wamekuwa wakichangia bajeti na mwisho wakishauri ama kuipongeza bila kuangalia bajeti husika ipo kwa ajili ya wananchi ama kwa ajili ya serikali na kudai kuwa wabunge wa CCM wanafanya kazi ya serikali badala ya kuwatetea wananchi waliowatuma bungeni.
DKT Slaa amewaonya wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kutumia dikshonari katika kupambanua kauli mbali mbali badala ya kutumia nguvu kusema wabunge wa Chadema wametukana bungeni na kusema wao wamesema kweli.
Hata hivyo aliwataka usalama wa Taifa kulinda raslimali za Taifa kama twiga wanaosafirishwa nje ya nchi badala ya kupambana na Chadema .
Alisema kuwa Chadema inawataka wabunge wa Chadema kupambana bungeni bila kurudi nyuma wala kutoa hata sentimita moja katika kupambana na spika.
Kwani waziri mkuu amekuwa ni mmoja kati ya viongozi wanaolidanganya bunge kwa kutoa mambo ya uongo bungeni badala ya kueleza ukweli .
Awaagiza wabunge wa Chadema kuchapisha vitabu vya manbo ya bungeni na kuvisambaza kwa wananchi ili kujua kinachoendelea na kuwataka kuwa wakali zaidi na hata kama spika Makinda atawafukuza basi awafukuze wote ili kufanya kazi na wananchi kama hii inayoendelea.
katika ziara hiyo DKt Slaa na wabunge watano waliosimamishwa bungeni Dodoma na naibu spika wa bunge Job Ndungai wameweza kuliteka jimbo la Iringa mjini .
Huku wakiapa kwenda jimbo la Njombe kusini linaloongozwa na spika wa bunge Anne Makinda ili kumchongea kwa wapiga kura wake kutokana na kushindwa kuongoza nafasi hiyo ya uspika na kuegemea kutetea ufisadi wa serikali ya Chama cha mapinduzi (CCM).
Huku kukosekana kwa mbunge Tundu Lisu na Lema kumeonyesha kuwasikitisha umati mkubwa wa wananchi walifika katika uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa kwa ajili ya kuwashuhudia wabunge wote watano waliosimamishwa hatua iliyopelekea mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa kuwaomba radhi wananchi
Akitoa utambulisho wa wabunge waliofika mwenyekiti wa Chadema Iringa mjini na mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Msigwa alisema kuwa wabunge hao wawili hahajabatatika kufika mkoani Iringa kutokana na kuwa katika majukumu ya kesi ya Godbless Lema na hivyo wamechelewa kufika japo katika mkoa wa Mbeya majemba haya yatakuwepo hali iliyowafanya mashabiki na wanachama wa Chadema kupaza sauti ya kuguna .
Hatua hiyo ilipelekea mbunge mchungaji Msigwa kuwaomba radhi na kuwahoji kama wamesamehe ama lah! na umati huo kupasa sauti kuwa hanawa shaka na hilo na kuwa wamesamehe.
Akitoa salam zake kwa wakazi wa jimbo la Iringa mjini mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi ( MR SUGU) alisema kuwa serikali ya CCM imepotezana na waoa kama wapinzani wanamshangaa waziri mkuu Mizengo Pinda kumchukia mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (CCM) kwa kuonyesha kusimamia ukweli kwa kuipinga bajeti ya waziri mkuu na kueleza ukweli kuwa serikali ya CCM imevaa miwani ya mbao .
Alisema kwa kuwa CCM imezoea kusifiwa kwa kila jambo waziri mkuu alitegemea kuwa mbunge Filikunjombe angeunga mkono bajeti hiyo kama ilivyo kwa wabunge wengine wa CCM na kuwa kutokana na kuwa tofauti waziri mkuu Pinda alionyesha kutofautiana na Filikunjombe kwa mtazamo wake kuwa ni mpinzani .
" Nawaelezeni wana Iringa kuwa mimi kila mmoja ananitambua kuwa ni msela na nimetoka kijiweni na hivyo nitawawakilisha watanzania wenzangu kisela ila kamwe sitaunga mkono hoja ambazo binafsi naona hazipo kwa ajili ya kumsaidia mwananchi wa hali ya chini binafsi nampongeza mbunge Filikunjombe kwa kuwa si mnafiki kama wengine "
Sugu alisema kuwa suala la wao kufukuzwa bungeni kwa siku tano kwa kuomba miongozo ya spika si jambo la hatari sana na kuwa kwa kawaida mbunge anaweza kuomba mwongozo wa spika hadi mara 20 kama wabunge wengine wamekaa kimya na si kosa kuomba mwongozo ila kwa spika Makinda na Ndungai wao wanaona kama ni kesi .
Kwani alisema kuwa kosa kubwa la wao kufukuzwa bungeni ni kuomba mwongozo wa spika na naibu spika Ndungai aliona kama ni kosa na kuwafukuza huku akimwacha mbunge wa CCM Selukamba akitumia lugha ya matusi zaidi kuendelea kuwepo
Hata hivyo alisema kuwa mbinu ya kiti cha spika kutaka kukilinda chama tawala wao kama wabunge wa Chadema wamezidungua na hivyo hawatasita kuomba mwongozo na iwapo spika Makinda na Ndungai watachukia basi kimpango wao .
Alisema kuwa wanamshangaa waziri Pinda kumkana mbunge Filikunjombe kwa sababu ya kusema ukweli na kuwa serikali ya CCM na spika wamekuwa wakiwapenda wabunge wanaosifia kila jambo bila kuangalia mateso ambayo wananchi wanyonge wanayapata.
Hata hivyo aliwashukia usalama wa Taifa kuwa ni watu ambao wapo kwa ajili ya kutazama usalama wa CCM badala ya kuangalia usalama wa Taifa kwa kuangalia amani ya Taifa bila kuegemea chama tawala.
Alisema iwapo usalama wa Taifa wapo basi wangewezesha kuwapata watu waliohusika katika shambulio la mhariri mtendaji wa NEW Habari 2006 Ltd Absoloom Kibanda ila kwa kuwa kila jambo baya wamekuwa wakilielekeza Chadema na zuri CCM basi ni vigumu kueleza ukweli.
Mbunge huyo alisema kutokana na hatua ya Spika kuwatimua bungeni wao wamepanga kwenda jimboni kwa spika Makinda ili kumchongea kwa wapiga kura wake kutokana na udhaifu mkubwa anaoonyesha bungeni katika kusimamia bunge .
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ilemela mkoani Mwanza , Highness Kiwia alisema kuwa pamoja na bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwa na wabunge zaidi ya 300 ila wabunge ambao wamekuwa wakitetea wananchi ni wabunge wa Chadema pekee .
Kwani alisema kuwa wabunge wa CCM wanatetea ufisadi wa serikali yao na kutaka chenji ya rada badala ya kuwasaka wahusika wa ufisadi huo wa rada na kuwa sasa umefika wakati wa wao kudai haki kwa nguvu zote na ikiwezekana hata kumwaga damu kwa ajili ajili ya Taifa .
STORI NA PICHA ZOTE: FRANCIS GODWIN
0 maoni:
Post a Comment