Mh. Namelok Moringe Sokoine akikabidhiwa cheti cha kushiriki mbio za Edward Moringe Sokoine Mini Marathon na mkuu wa mkoa wa Arusha mh. Magesa Mlongo jana wilayani Monduli Arusha.
Namelok Sokoine ni binti wa hayati Moringe Sokoine ambaye ni mfano wa kuigwa na wanawake wote nchini kwa kusimama kidete katika maandalizi ya kumbu kumbu za baba yake, aliyefariki mnamo tarehe 12/4/1984 kwa ajali ya gari wakati huo akiwa ndiye Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania.
Viongozi wa kitaifa na Mkoa, pamoja na mtoto wa Hayati Sokoine wakitembea kuelekea eneo la kuanzia mbio za riadha
Kutoka kushoto ni Mh Namelok Sokione,Waziri Mukangara, Mh Lowassa, Mh Ole Sendeka na Mh Julius Kalanga.
Baadhi ya washiriki wa riadha katika mavazi ya kiasili
Mhe: Olesendeka akishiriki mbio za Mini Marathon ya kumbu kumbu ya hayati "Edward Moringe Sokoine 2013" Wilayani Monduli siku ya jana.
Mh Lema aliyevalia gwanda la kaki na namba kifuani akiwa katika mstari wa kuandikishwa baada ya kumaliza mbio kilometa 2 za Mini Marathon ya kumbu kumbu ya hayati "Edward Moringe Sokoine 2013" Wilayani Monduli siku ya jana. Mbele yake ni Seria mwenye blog ya Arusha 255 akiwa nae kashiriki mbio hizo.
Mhe: Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenela Mkangala akiwahutubia mamia ya watu walio hudhuria siku ya kumbu kumbu ya kutimiza miaka 29 ya hayati waziri mkuu "Edward Moringe Sokoine" huko Monduli
Waziri Mkangara aliwaomba wananchi kuikumbuka siku aliyofariki Edward Sokoine 12/4/1984 pamoja na mema aliyowatendea wananchi wake.
Waziri Dr Fenela Mkangala (wakwanza kushoto), akifuatia Edward Lowasa (MB), katikati ni Binti wa Hayati Sokoine ambaye ni Namelok Sokoine (MB), akifuatiwa na Olesendeka (MB). wakishuhudia tukio lambio likianza rasmi.
Viongozi na wanafamilia wakishuhudia matukio ya michezo yaliyokuwa yakiendelea.
Wairi Mkangara akiwa na wabunge wakati wa mbio za Mini Marathon ya kumbu kumbu ya hayati "Edward Moringe Sokoine Mini Marathon 2013" Wilayani Monduli siku ya jana.
Mbunge wa Jimbo la Arusha-Chadema,Mh. Godbress Lema akishiriki mbio za kumuenzi Waziri Mkuu wa zamani,Hayati Edward Moringe Sokoine (Edward Moringe Sokoine Mini Marathon 2013) zilizofanyika kijijini kwake Monduni Juu,Mkoani Arusha
Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiweka shada la Maua kwenye Kaburi la hayati Edward Moringe Sokoine,aliefariki miaka 29 iliyopita
Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenela Mukangala akiweka shada la Maua kwenye Kaburi la marehemu Edward Moringe Sokoine
Wake wa Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine wakiweka shada la Maua juu ya kaburi
Baadhi ya Bloga wa Arusha wakiwa Monduli Juu kunasa matukio mbalimbali katika maadhimisho hayo. Lutoka kushoto ni Victor Machota wa Asili Yetu Tanzania, Emanuel Gadiola wa Wazalendo 25 Blog na wa mwisho ni bosi munene wa Arusha255 “noise of silence” Tumaini Seria. Blogu nyingine kwa Arusha ni pamoja na LIBENEKE LA KASKAZINI, BERTHA BLOG, Jamii Press, na Jamii Blog zikitajwa kwa uchache. PICHA NA VICTOR MACHOTA, SERIA JR, NA WOINDE SHIZZA
0 maoni:
Post a Comment