Mida ya jioni kama saa kumi na mbili kasorobo Mwandishi wa Habari wa BBC Bw. Jayson amekamatwa Loliondo kwenye mkutano uliododa wa Mwigulu Nchemba uliopo kata ya Waso.
Inasemekana mwandishi huyo alikamatwa baada ya kugundulika alikuwa anafanya uchunguzi kuhusu migogoro kati ya Wamasai wa Loliondo na Mwaarabu anayejulikana kwa jina la Ortelo. Kwenye mkutano huo wamama wa kimasai walimrushia Mwigulu kadi za ccm huku wamepandwa na hasira.
taarifa zinaeleza zaidi kuwa, ilipo fika mida ya moja kasorobo Tundu Lissu aliweza kuombea mwandishi wa BBC aliyekamatwa Bw. Jayson, Tundu Lissu ambaye naye alikuwa na mkutano huko ameamua kutoka Soitsambu kwenda kumtetea na kuhoji sababu za mwandishi wa habari kukamatwa.
Waandishi wengine wa habari Ramadhan Mvungi wa Startv na Musa Juma inasadikiwa wamekimbilia porini baada ya Mwigulu kuagiza wakamatwe, akihoji nani aliwaita kwenye mkutano wake!
Chanzo: Media 2 Solution
0 maoni:
Post a Comment