Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TBL YAKABIDHI KISIMA CHA SH. MIL. 51 KIJIJI CHA MAKANYA SAME

Mhandisi wa Kampuni ya Dr Gogo engineering limited, Godwin Kalaghe (kulia), akimkabidhi Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo nyaraka za taarifa za kukamilika kwa ujenzi wa kisima cha maji katika Kijiji cha Makanya, wilayani Same juzi. Ujenzi wa kisima hicho uliogharimu sh. mil. 51.6 ulifadhiliwa na TBL.

Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo akisaidia kumtwisha ndoo ya maji mkazi wa Kijiji cha Makanya, wilayani Same, Asia Zuberi ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi wa kisima cha maji kwa msaada wa TBL kwa gharama ya sh. mil. 51.6. Hafla hiyo ilifanyika kijijini hapo juzi.

Mradi wa kisima cha maji kilichofadhiliwa na kampuni ya bia Tanzania katika kijiji cha Makanya wilayani Same chenye thamani ya shilingi milioni 51.6.Uwepo wa kisima hiki utasaidia kupunguza tatizo la maji hususani kwa wakazi wa Tambarare katika wilaya ya Same

Chanzo: HAKI NGOWI.COM

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO