Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Dola mil 158 zahitajika kutatua tatizo kubwa la maji safi linalolikabili Jiji la Arusha

KIASI cha dola milioni 158 kinahitajika ili kutatua tatizo kubwa la maji safi linalolikabili Jiji la Arusha na kusababisha wananchi wengi kutegemea maji ya visima na wengine kutembea umbali mrefu kuyafuata.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Arusha, Injinia Ruthi Koya alisema kupatikana kwa kiasi hicho cha fedha ndiko kutatatua tatizo la maji.

Alisema mamlaka hiyo haina kiasi hicho cha fedha kwa sasa bali inategemea ruzuku ama mkopo ili kuweza kumudu kutatua tatizo la maji linalozidi kulikabili jiji hilo, hasa baada ya kuongezewa maeneo kutoka wilayani Arumeru.

Injinia Koya alitaja maeneo ambayo hadi sasa hali ya upatikanaji maji si nzuri ni pamoja na Olasity, Kwa Mrombo, FFU na baadhi ya maeneo ya Mianzini ambapo jitihada zinafanywa kupunguza makali hayo.

Alifafanua kuwa baada ya mamlaka hiyo kuchimba kisima kirefu katika eneo la Sombetini, wanatarajia kuyasambaza maji hayo katika maeneo ya Olasity na Kwa Mrombo ambako kuna tabu kubwa ya maji.

Alisema uwezo wa mamlaka hiyo kwa sasa ni kuzalisha lita za ujazo milioni 45,000 kwa siku huku mahitaji halisi yanayotakiwa ni lita milioni 93,270 kwa siku hivyo kuwa na changamoto kubwa ya kufikia malengo hayo.

Aliomba wananchi kumvumilia kwa kipindi cha miaka mitano kuweza kutatua changamoto hiyo ya upatikanaji maji safi na huduma ya uondoaji maji taka mjini.

Tanzania Daima

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO