Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

BREAKING NEWS: RCO GEITA AFARIKI KWA AJALI YA GARI; ANGALIA PICHA ZA AJALI HUMU

Afisa Upelelezi wa Polisi Mkoa wa Geita (RCO) SSP-Magnus Mng’ong’o amefariki dunia baada ya gari alilokuwa akisafiria kugongana na Roli la kubeba Samaki majira ya saa 4 usiku eneo la Chibingo katika barabara ya Geita Bukoba wakati akitoka eneo la Katoro kikazi.

Tunaendelea kufuatilia taarifa zaidi na tutakujuza hapa hapa baadae kidogo…..

Chanzo: G Sengo Blog

MORE UPDATES

Magari yaliyogongana mkoani GEITA na kusababisha kifo cha aliyekuwa mkuu wa upelelezi wa Makosa ya jinai,SSP MAGNUS BONIFACE MNG'ONG'O 13/04/2013 katika Kijiji cha Chibingo kata ya Nyamigota Barabara ya Geita – Chato.

 

 

Gari no T.467 ANG MITISUBISH FUSO,iliyokuwa ikiendeshwa na SAID KHALIFANI,MIAKA 38.Mkazi wa Mwanza,iligongana na Gari no.429 BMN TOYOTA COLLORA iliyokuwa ikiendeshwa na MAGNUS BONIFACE MNG'ONG'O mkuu wa upelelezi wa Geita.

Aidha mkuu wa upelelezi alikuwa kazini akitokea Wilaya ya Chato-Buselesele akielekea Geita mjini,akiwa njiani ndipo alipo pata ajali.

Alifariki wakati akipatiwa matibabu,katika hospitali ya wilaya ya Geita usiku,chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa na katika ajali hiyo hakuna majeruhi,Hata hivyo dereva wa Fuso anashikiliwa kwa upelelezi.

Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda nyumbani kwao kwa mazishi mkoani  IRINGA.

Taarifa yake Kaimu Kamanda wa polisi,

Kamishina Msaidizi wa polisi,

JAPHET J.LUSINGU.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO