Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MSIBA WA BILIONEA BABU SAMBEKE WAWA GUMZO JIJINI ARUSHA…VIGOGO WATAWALA MSIBANI–ANGALIA MATUKIO HAPA

DSCF8833

Jamal Sambeke mtoto wa marehemu akifunga jeneza la baba yake mara baada ya watu mbalimbali kutoa heshima zao za mwisho nyumbani kwake njiro Themi Mkoani Arusha

DSCF8840

Waombolezaji wakibeba jeneza la Bilionea Babu na kuweka kwenye gari maalumu tayari kwa safari kuelekea Moshi kwa mazishi

DSCF8828

Watu wakitoa heshima za mwisho

DSCF8844

Watoto wa marehemu Sia na Getrude waliovalia nguo nyeupe

DSCF8834

Jamal akifunga jeneza la marehemu Babu Sambeke

DSCF8830

Jaji Aisha nyerere msibani pamoja na mkurugenzi wa kibo palace Vicent Laswai

DSCF8832

DSCF8848

Baadhi ya magari ya kifahari yaliyofika katika msiba huo

DSCF8838

Mkurugenzi wa hoteli ya Kibo Palace Vicent Laswai akizungumza msibani mara baada ya watu mbalimbali kutoa heshima zao za mwisho

DSCF8847

Waombolezaji

Mamia ya vigogo pamoja na watu mbalimbali wafurika nyumbabi kwa marehemu Bilionea “Babu Sambeke”Ernest Sambeke eneo la njiro jijini Arusha kuaga mwili wake unaotarajiwa kuzikwa kesho nyumbani kwake eneo la Karanga mjini Moshi huku msiba huo ukiwa tofauti na misiba mingine iliyozoekeaka hapa Nchini

Marehemu,Sambeke alifariki hivi karibuni katika ajali ya ndege aliyokuwa akiiendesha na pia mmiliki wa ndege hiyo ambapo ilianguka katika eneo la Kisongo na kusababisha kifo chake Mkoani Arusha

Shughuli za kuaga mwili wa marehu zilikamilika majira ya saa 8:45 mchana huku mwili huo ukipakiwa katika gari maalumu la kifahari tayari kusafirishwa kuelekea nyumbani kwake Moshi kwaaajili ya mazishi

Taratibu za kuaga mwili wa marehemu zilianza majira ya saa 5 asubuhi huku wafanyabiashara wa madini pamoja wafanyabiashara wengine kutoka hapa Arusha na Moshi walionekana kutawala msiba huo.

Katika zoezi hilo la kuaga mwili wa mareheu Padri Florentine Mallya ambaye ni mdogo wa marehemu aliongoza misa ya kumuombea marehemu na baada ya kumaliza alitoa fursa kwa watu mbalimbali kupita mbele ya jeneza kwaajili ya kuaga mwili

Ndani ya jeneza marehemu alivalishwa nguo zake za kirubani huku ,baadhi ya wanajeshi kutoka jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) walionekana jana katika zoezi la kuuaga mwili wa marehemu ambapo baadhi yao walikuwa wamevalia sare za jeshi hilo

Hatahivyo,baadhi ya watu walionekana katika hali ya kawaida huku watoto wakionekana na nyuso za huzuni mda wote

Tofauti na misiba mingine nchini watu mbalimbali walipata fursa ya kupata chakula na vinywaji mbalimbali kwa kujihudumia vikiwemo vinywaji aina ya Bavaria ambapo watu waliohudhuria zoezi hilo walionekana wakijihudumia zaidi vinywaji vya bavaria

Magari ya kifahari yalionekana kutawala msiba huo huku barabara ya njiro ikionekana kuwa na msongamano kubwa iliyosababishwa na zoezi hilo la uwagaji wa mwili

Marehemu aliacha watoto watatu ambao ni Sia,Jamal,Getruda.

PICHA NA STORI: JAMII BLOG (PAMELA MOLLEL)

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO