KWA mujibu wa mashuhuda wa ajali iliyotokea leo majira ya sa 5 asubuhi Jijini Arusha, inakadiriwa zaidi ya watu 18 wamepoteza maisha kufuatia kufukiwa na gema la mchanga/moram wakati wakichimba na kupakia kwenye malori.
Ajali hiyo mbaya imetokea katika machimbo ya moram nje kidogo ya Jiji eneo la Moshono-Kiserian ambapo vijana hao wanaokadiriwa kufikia idadi hiyo walikuwa wakipakia moram kwenye magari mawili, moja ni Fuso na lingine Scania kubwa (tani 18) na yote mawili yamefukiwa kabisa na kifusi.
Shuhuda mmoja wa ajali ambae pia ni mchimbaji ameieleza Blog hii kwamba kwa kawaida gari ndogo kama Fuso hupakiwa na watu 7, na hiyo kubwa huwa na watu 12 bila kuhesabu dereva na utingo.
Blog hii iliweza kushuhudia sehemu ndogo sana ya Fuso ikionekana lakini gari nyingine ilikua imefukiwa kabisa na kupondeka vibaya.
Miongoni wa waliofikwa na mauti ni pamoja na madereva wa magari hayo. taarifa za eneo la tukio zinaeleza utingo mmoja ameokolewa akiwa amejeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali lakini dereva wake amefariki dunia.
Katika eneo la ajali hali ni ya simanzi na vilio toka kwa kina mama huku baadhi wa wababa na marafiki na ndugu wa jamaa waliofukiwa wakishindwa kujizuia na kuangua kilio.
Meya wa Manispaa Mh Gaudence Lyimo pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema ni miongoni mwa viongozi wakubwa waliofika eneo la ajali kusaidiana na kikosi cha Jeshi la Wananchi kufanya uokozi.
Blogu hii ilishuhudia pia Wachina wakipeleka moja ya mashine zao (Excavator) kuongeza nguvu katika kusaidia kufukua miili ya watu hao iliyonaswa na kifusi hicho.
Mwili wa dereva wa lori moja kubwa lenye ujazo wa tani 18 ukiwa umeopolewa na askari jeshi, tayari kupelekwa mochwari ya Hospitali ya Mt Meru. Dereva huyu ametambulika kwa jina moja tu la Alex amefikwa na mauti akiwa ndani ya gari hilo wakati vijana wengine wakiendelea kupakia moram asubuhi ya leo
Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema akiwasili eneo la ajali mapema asubuhi
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia ajali hiyo mbaya wakishangaa zoezi la uokoaji na wengine wakisubiri kutambua ndugu zao, jambo ambalo halikupata nafasi
Meya wa Manispaa ya Arusha, Mh Gaudence Lyimo akisaidiana na vikozi vya jeshi katika zoezi la uokozi
Mh Lema akiangalia namna vikosi vya Jeshi la Wananchi pamoja na askari Polisi wakiendelea na zoezi la uokozi
Mwananchi huyu aliishiwa nguvu baada ya kushuhudia mwili wa rafiki yake ukiopolewa kutoka kwenye kifusi
Kina mama wakilia kwa uchungu wakihofu kuondokewa na wapendwa wao
Vikosi vya Jeshi la Wananchi na Polisi vikiwa kazini
Sehemu ndogo ya Fuso ikionekana huku gari nyingine ikiwa haionekani kabisa
Ambulance ya Jiji tayari tayari kwa lolote ikihitajika
Wachina wakielekea eneo la jali na vifaa vyao kusaidia zaidi zoezi la uokozi
Wanajeshi zaidi wakielekea chini kwenye mgodi
Tunaomba radhi kwa ubora hafifu wa picha hizi….
0 maoni:
Post a Comment