Kufuatia kuporomoka kwa gema la mwamba jana na kufukia wachimbaji wanaokadiriwa kufikia 18 Jijini Arusha, katika machimbo ya moram yaliyoko eneo la Moshono, Mkuu wa Mkoa, Magessa Mulongo aliagiza machimbo yote ya mchanga kufungwa hadi hapo serikali itakapotoa amri ya kuendelea na shughuli za uchimbaji
Tukio kama hili liliwahi kutokea mwaka 1997 ambapo watu 7 walipoteza maisha na uongozi wa Jiji uliwaagiza wachimbaji kutumia katapila badala ya mikono, jambo ambalo halikutekelezwa ipaswavyo.
Hata hivyo wananchi waliishutumu vikali serikali kwa kushindwa kuboresha miundo mbinu ya eneo hilo kwa kuwa tukio kama hilo si mara ya kwanza kutokea hivyo walidai kuwa ni uzembe wa hali ya juu
Hadi kufikia jana jioni, maiti za watu 13 ndiyo zilikuwa zimeopoelewa wakati watu wawili tu ndiyo walikuwa wametoka wakiwa hai na kukimbizwa katika Hospitali ya Mt Meru kwa ajili ya matibabu kutokana na kuvunjika miguu.
Waliotolewa wakiwa hai walitambuliwa kuwa ni Matei Nenano na Lushooki Laizer wote wakazi wa jijini Arusha.
Maiti zilizoopolewa ni za mmiliki wa magari ya kubeba kifusi hicho, Julius Peter, Alex Mariaki, Gerald Lutakata, Hassan Hamis, Sauli Raphael, Bariki Revelian na Kababuu Ruafela.
Wengine ni Mwenda Kiboliboli, Japhet Jivaline, Benard Masai, Gerald Jacob, Fredy Losileani, Julius Palangyo na mtu ambaye alijulikana kwa jina moja la Christopher.
Watu walioshuhudia tukio wanasema ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 5.00 asubuhi wakati shughuli za uchimbaji zikiendelea huku mvua inanyesha, na ndipo ghafla gema la mwamba liliporomoka na kuwafunika.
Taarifa mpya kwa leo zinaeleza kwamba zoezi la utambuzi wa miili ya marehemu unatarajiwa kufanyika leo katika Hospitali ya Mt Meru.
Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Mh Joshua Nassari, wote kutoka CHADEMA wakisaidiana na askari jeshi kufanya uokozi wa miili ya marehemu jana mchana.
mmoja wa miili ya marehemu ikitolewa kwenye kifusi
Mh Lema akihojiwa na waandishi wa habari katika eneo la ajali
Kichwa cha Scania tani 18 kikianza kuonekana baada ya kufukuliwa
Wabunge wa Chadema, Arusha Mjini na Arumeru Mashariki wakifuatilia tukio la uokozi
Scania kama linavyoonekana baada ya kufukuliwa
Picha zote na Arusha255 Blog “Noize of Silence”
2 maoni:
Poleni sana ndugu zetu wa Arusha roho zinauma sana kwa matukio kama haya lakini tufanyaje????????? Kazi ya mola haina makosa......muangu ilaze mahali pema peponi roho za marehemu..........tupo pamoja ktk wakati huu mgumu.........amen
Poleni kwa yaliyowakuta ila tuzidi kumwomba mwenyezi Mungu atuepushie matatizo kama hayo,,, Amen
Post a Comment