Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Waziri Mkuu Pinda Ahudhuria Misa ya Pamoja Jijini Arusha Kuaga Marehemu Waliofikwa na Mauti Baada ya Kufukiwa na Kifusi Jana.. Awafariji Wafiwana na Kusaini kitabu cha Maombolezo

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Peter Pinda hii leo aliungana na waombolezaji wengine katika misa ya pamoja kuaga miili ya vijana waliokufa kwa kuangukiwa na gema la mchanga maeneo ya Moshono jana, Jijini Arusha.

Mh Pinda baada ya kumaliza tukio hilo, yeye na msafara wake muda huu wakaelekea yaliko machimbo hayo yaliyoleta maafa..

Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitia saini kitabu cha maombolezo alipofika  mkoani Arusha leo Kuwapa pole ndugu na jamaa ambao ndugu zao wamefariki katika machimbo ya  Moramu katika eneo la Moshono Mkoani Arusha. Maporomoko hayo yametokea jana na kusababisha vifo vya watu13  na majeruhi wawili ambao mmoja ameruhusiwa na mwingine amelazwa katika Hospitali ya Mount Meru

Waziri Mkuu akiwa na wabunge wa Arusha na Meya pamoja na mkuu wa mkoa kwenye msiba huo mzito. Toka Kushoto ni Mbunge wa Arusha Mjini Mhe Godbless Lema, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Magessa Mulongo, Meya wa jiji la Arusha Mstahiki Gaudence Lyimo, Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe Joshua Nassari na Mbunge wa kuteuliwa Catherine Magige

Sehemu ya majeneza ya marehemu katika ibada hiyo maalumu leo

Waziri mkuu Mizengo pindaakiongea na familia, ndugu na jamaa wa marehemu walioporomokewa na moramu.


Kiongozi wa dini akiombea marehemu waliofariki kwa kuporomokewa na Moramu

Waziri Mkuu akipeana mkono na Askari wa Jeshi la Wananchi (jwtz) alipotembelea eneo la tukio. 

Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipowasili mkoani Arusha leo Kuwapa pole ndugu na jamaa ambao ndugu zao wamefariki katika machimbo ya Moramu katika eneo la Moshono Mkoani Arusha, maporomoko hayo yametokea jana nakusababisha vifo vya watu 13 na majeruhi wawili ambao mmoja ameruhusiwa na mwingine amelazwa katika Hospitali ya Maunti meru.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoka eneo la tukio katika machimbo ya Moramu katika eneo la Moshono Mkoani Arusha,  maporomoko hayo yametokea jana nakusababisha vifo vya watu 13 na majeruhi wawili.

Picha zote na Chris Mfinanga

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO