Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Askari Polisi ajichomeka UVCCM

ASKARI namba F 7961 PC Stanley Mdoe, anayefanya kazi katika kituo cha polisi Mvomero mkoani Morogoro, anadaiwa kujihusisha na siasa kwa kuingia kwenye kugombea ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa kupitia kundi la vijana.

Chanzo chetu kilieleza kuwa, askari huyo anayejitambulisha kama mtoto wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, akijitambulisha kwa jina la Stanley Bendera, alikamatwa mkoani Dodoma juzi jioni wakati uchaguzi wa UVCCM ukiendelea.

Kwamba akiwa amevalia sare za chama hicho tangu siku ya kwanza akiomba kura kwa wajumbe, huku akiwa amepamba gari yake kwa picha zake, baadhi ya wanachama wanaomfahamu waliwatonya maafisa usalama waliokuwepo eneo hilo.

Tanzania Daima ilitonywa kuwa maafisa hao nao walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi mkoani Dodoma ndipo alipotiwa mbaroni.

Aidha, askari huyo pamoja na juhudi zake za kusaka ujumbe wa NEC, lakini hakushinda.

Kumekuwa na mkanganyiko kuwa askari huyo tayari aliomba likizo isiyokuwa na malipo, lakini taarifa nyingine zinasema aliacha kazi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, alisema kuwa hana taarifa ya askari huyo kujihusisha na masuala ya kisiasa.

Shilogile alisema kuwa alipata taarifa za kukamatwa kwa askari huyo mkoani Dodoma, na kwamba yeye alikuwa akimtafuta kwa shughuli za kikazi kwa muda wa siku mbili bila kumpata.

Source: Tanzania Daima, 25 Oktoba 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO