Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

DC Mrisho Gambo apandishwa kizimbani

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wilaya ya Korogwe leo (jana) imemkataa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kumwakilisha Mkuu wa wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo katika kesi ya madai ya sh.Milioni 96 dhidi yake.

Katika kesi hiyo Na. 7/ 2012 mlalamikaji ni Mwanasheria wa halmashauri ya Mji Korogwe, Najum Tekka anayedai kukashifiwa na Gambo wakati wa kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya kwamba stashahada ya Sheria aliyopata mtumishi huyo niya chupi.

Awali ilidaiwa kwamba mkuu huyo alimwalika mlalamikaji kutoa ushauri wa kisheria kuhusu namna ya kumaliza mgogoro baina ya halmashauri ya mji na wafanyabiashara na kwamba baada ya kufanya hivyo mlalamikiwa alipinga ushauri uliotolewa na kIsha kutoa kauli hiyo kwamba shahada yake ni ya chupi.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Hamis Salum mlalamikaji huyo aliiomba mahakama imwondoe mwanasheria mkuu wa serikali ambaye aliwakilishwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali, Rebecca Msalangi kwakuwa hana mamlaka katika madai hayo na kamwe ofisi yake haikuwahi kupeleka ombi maalum la kutaka kumwakilisha Gambo kwenye shauri hilo.

Kwa upande wake Hakimu Mkazi akisoma uamuzi mdogo wa mahakama kuhusiana na mabishano hayo alikiri kwamba utaratibu haukufutwa na kamwe hapakuwa na ombi la mwanasheria mkuu wa serikali kutaka kumwakilisha Gambo kwenye madai hayo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 14 mwaka 

Source: WotePamoja.Com

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO