MWANARIADHA mahiri wa zamani na Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) hivi sasa, Meja mstaafu Filbert Bayi, amefanikiwa kuchaguliwa kuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiwakilisha Wilaya ya Karatu mkoani Arusha.
Bayi amefanikiwa kukata tiketi hiyo kupitia uchaguzi uliofanyika hivi karibuni, baada ya kupata kura 264, ambapo ataungana na Mary Sulley kura 545, Ori Pembe (kura 460), Fabiola Deo (kura 456) na Amsi aliyepata kura 322.
Katika uchaguzi huo, nafasi ya uenyekiti wa wilaya, ilikwenda kwa Mustafa Mbwambo aliyepata kura 512 na kumwangusha Gerald Gwaha aliyepata kura 148, huku mgombea mwingine aliyefahamika kwa jina la Tippe akijitoa katika kinyang’anyiro hicho.
Kwa upande wa nafasi ya Halmashauri Kuu (NEC), Awaki Tlemai, alishika nafasi ya kwanza kwa kupata kura 545 akifuatiwa na Daniel Ilakwahhi kura 114.
Source: Dina Ismail
0 maoni:
Post a Comment