Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, Oktoba 10, 2012, jijini Dar es Salaam kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali kufuatia kubainika kwa matumizi ya dawa bandia za kupunguza makali ya Ukimwi zenye jina la Biashara TT –VIR 30.
Mmmoja wa maafisa kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini (TFDA) ambaye hakutaka jina lake liandikwe kwenye vyombo vya habari akiwaonyesha waandishi wa habari Dawa badia za kupunguza makali ya Ukimwi (ARVS) zilizoondolewa katika vituo vya kutolea huduma mara baada ya kugundulika.
Makopo ya dawa za kupunguza makali ya Ukimwi yakitofautiana vifungashio. Kopo la kwanza kushoto linaonyesha dawa halisi ya kupunguza makali ya Ukimwi iliyokidhi viwango ikifuatiwa na makopo matatu yenye dawa bandia ya kupunguza makali ya Ukimwi yenye jina la biashara TT –VIR 30 toleo namba 0c.01.85 yaliyotengenezwa na kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd. (Picha na Aron Msigwa – MAELEZO)
0 maoni:
Post a Comment