Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Vipaji Toka Moyoni… Miraji na kipaji cha uchoraji michoro ya Tingatinga

Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zinakabiliwa na tatizo kubwa la ajira kwa vijana. Serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo wamekuwa wakiimiza vijana kufikiria zaidi kujiajiri badala ya kukaa na kusubiri kuajiriwa.

Hata hivyo, zoezi la kujiajiri humlazimu mtu kuwa na aidha kipaji au uwezo wa kubuni mradi wa biashara na kuusimamia kwa faida ili kujipatia kipato, au kutumia kipaji alichonacho kwa ajili ya kuzalisha bdihaa ama huduma fulani ambayo itamuwezesha kujipatia kipato.
Miongoni mwa vijana ambao wameweza kutumia vipaji vyao katika kujitafutia riziki ni Miraj Ally Abbas ambae hujishughulisha na uzalishaji wa bidhaa za mapambo na vivutio kwa watalii wanaotembelea Jiji la Arusha.
Miraji ni mchoraji mzuri wa michoro ya “Tingatinga ambayo iliasisiwa Mtanzania mmoja aliyefahamika kwa jina la Hayati Edward Said Tinga Tinga aliyeanza kuchora michoro ya kawaida katika mwaka 1968 hadi alipofariki 1972 jijini Dar es Salaam kwa kupigwa risasi kwa kudhaniwa jambazi na kuzikwa katika makaburi ya Msasani Mikoroshini. Michoro hii imekuwa ikichorwa kwa miaka 41 sasa na kuweza kuingia katika ramani ya dunia na kuwa na jina kubwa.
Blog hii imeweza kutembelea eneo ambalo miraji anafanyia shughuli zake hapa Arusha, eneo ambalo ni maarufu kwa uuzwaji wa picha za michoro ya Tinga Tinga na bidhaa nyingine za kiasili; AFRI HOPE HADCRAFT INDUSTRY & CURIO SHOP jirani na jengo jipya la NSSF Arusha, Barabara ya Old Moshi.
Muasisi wa michoro hii, Said Tinga Tinga alizaliwa katika Kijiji cha Nakapanya, zamani kikiitwa Namuchalia, kilichopo katika Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma. 
Kwa mujibu wa maelezo ya Miraji, michoro yake mingi huuzwa kwa kuanzia Dola 20 hadi 100 kulingana na ukubwa na dizaini ya mchoro, ambapo wateja wengi ni wageni kutoka nje ya Afrika na mauzo hutegemea wingi wa wageni wanaotembelea eneo lao hilo.
DSCN5988AFRI HOPE Handcraft Industry & Curio Shop, duka maalumu kwa bidhaa za utamaduni na utalii lililopo pembezoni mwa barabara ya Old Moshi jirani na jengo jipya la NSSF Arusha. Hapa ndipo Miraji Ally Abbas na wenzake hufanyia shughuli zao.
DSCN5989Kijana Miraji Ally Abbas akiwa katika shughuli ya uchoraji kama alivyonaswa na kamera yetu. Mwenyewe amejitambulisha kama “KIPAJI TOKA MOYONI” na anapatikana kwa simu namba 0719 163770!
DSCN5990Miraji akiendelea na uchoraji, nyuma yake ni kijana mwingine aliyejitambulisha kama “Saami” Smwel Daimu ambae nae huchora michoro ya tingatinga katika eneo hilo pia.
DSCN5991Moja kati ya kazi za Saami
DSCN5992
DSCN5993Saami akiandaa mazingira ya kuanza kazi ya uchoraji..
DSCN5995Miraji katika hatua za mwisho kumalizia mchoro wake…
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO