Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Maelfu waungana na Heche kumsindikiza mgombea wa Chadema aliyeshinda rufaa ya Ubunge Sumbawanga Mjini

IMG-20121011-WA0002Heche akihutubia Sumbawanga Mjini jana

IMG-20121011-WA0003Maelfu ya wafuasi, wapenzi na wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) chini ya kamanda wake ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la chama hicho, John Heche leo jioni waliuteka mji wa Sumbawanga Mjini kwa shamrashamra za kumsindikiza mgombea wa chama hicho katika Jimbo hilo Norbet Yamsebo ambae ameibuka kidedea ktika rufaa iliyofunguliwa na mgombea wa CCM Awshy kupinga kuvuliwa Ubunge na Mahakama baada ya kupatikana na hatia ya kukiuka taratibu za uchaguzi.

IMG-20121011-WA0001Wananchi wa Kijiji cha Tamasenga wakilizuia gari alilopanda John Heche na kumlazimisha awahutubie, tukio ambalo lililazimisha msafara mzima kusimama eneo hilo kutii kiu ya wananchi.

IMG-20121011-WA0005

IMG-20121011-WA0007Awali kulikuwa na wasiwasi wa uwezekano wa kuibuka vurugu zilizopangwa makusudi dhidi ya CHADEMA huko Rukwa eneo la Mazwi Sokoni kutokana na shamra shamra kuanza mitaani na tetesi mbali mbali za wanachama na wapenzi wa CHADEMA kuanza kuandaa mapokezi ya Mh Norbert Yamsebo ambaye aliingia Mjini Sumbawanga akitokea Dar es Salaam, mapokezi ambayo yalipata mvuto zaidi kutokana na ushiriki kiongozi mkuu wa vijana wa chama hicho  John Heche.

Blog hii ilipata taarifa za tahadhari kwa viongozi wa Chadema kuwa kuna baadhi ya watu hawakufurahishwa na kitendo cha Mahakama kutupilia mbali rufaa kwa upande wao. Taarifa ilieleza kuwa kulikuwa na mpango wa Lori  kuvamia na kusababisha ajali likilenga gari linaloaminika kutumika na Heche na Yamsebo na kwamba hilo likishindikana basi mkutano ungevamiwa na kutokea fujo ya aina yoyote kutoka kwa watu walioandaliwa kupigana katika msafara wa mapokezi wakiwa na muonekano wa taswira ya kama vijana wa Chadema wakipigana wenyewe kwa wenyewe na hata kumdhuru mmoja ama wote kati ya viongozi walioambatana na msafara wa Heche.
Jambo la kushukuru ni kwamba mapokezi na mkutano huo vilimalizika salama tofauti na wasiwasi huo uliowatanda baadhi ya wafuasi wa chama hicho.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO