Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

NCAA yawekeza bil. 21/- za maendeleo

MAENDELEO wilayani Ngorongoro yameanza kushika kasi baada ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kuwekeza sh bilioni 21 kwa ajili hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya utekelezaji ya NCAA, miongoni mwa miradi ambayo imekamilika ni pamoja na ujenzi wa nyumba za kisasa, umeme, maji, ujenzi wa shule na hospitali, barabara na miundombinu kwa ajili ya kuhudumia watalii wanaofika eneo hilo.

Baadhi ya miradi iliyotajwa ni ujenzi wa nyumba za watumishi nje ya eneo la mamlaka uliogharimu sh bilioni 2.4, ujenzi wa nyumba za ghorofa katika makazi ya Kamyn Estate sh bilioni 2.6, ujenzi wa ofisi kuu sh bilioni 1.5, mradi wa umeme kutoka eneo la Loduare hadi makao makuu ya NCAA sh bilioni 3.5.

Mradi mwingine wa kipekee katika eneo hilo maarufu kwa utalii duniani, ni kituo cha kisasa kabisa cha polisi na cha mfano nchini kwa ajili ya kuimarisha shughuli za ulinzi na usalama.

Katika sekta ya elimu, mbali ya kujenga madarasa ya kisasa katika maeneo tofauti, NCAA pia inasomesha watoto 3,207 kutoka jamii za wafugaji ambao ni wakazi wa eneo hilo na yale ya jirani. Kati ya wanafunzi hao, wasichana ni 1,091 na wavulana ni 2,116.

Ngazi za elimu wanazosomeshwa watoto hao ni elimu ya msingi (kwa watoto wenye ulemavu), elimu ya sekondari, vyuo vya ufundi (VETA), vyuo vya kati (NACTE) na vyuo vikuu.

Mbali na kuchangia katika miradi ya maendeleo na ile ya ujirani mwema, NCAA imefanikiwa kusimamia na kuhifadhi rasilimali za hifadhi na uasilia wa hifadhi umeweza kulindwa licha ya kuwapo changamoto kadhaa.

Source: Tanzania Daima

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO