TAKWIMU ZA MECHI
KIKOSI CHA ARSENAL: Mannone, Jenkinson (Gnabry 82), Mertesacker, Vermaelen, Andre Santos, Ramsey, Coquelin, Arteta, Podolski (Arshavin 82), Cazorla, Gervinho (Giroud 75).
BENCHI: Shea, Koscielny, Djourou, Chamakh.
NJANO: Vermaelen, Arteta, Ramsey, Gervinho.
KIKOSI CHA SCHALKE 04: Unnerstall, Uchida, Howedes, Matip, Fuchs, Hoger (Jones 46), Neustadter, Holtby (Barnetta 65), Afellay, Farfan, Huntelaar (Marica 87).
BENCHI: Hildebrand, Moritz, Draxler, Kolasinac.
NJANO: Afellay, Hoger.
WAFUNGAJI WA MABAO YAKE: Huntelaar 76, Afellay 86.
MAHUDHURIO: 60,049
REFA: Jonas Eriksson (Sweden)Huntelaar akifungaMikel Arteta akisikitikia kipigoIbrahim Afellay akiifungia la pili SchalkeLukas Podolski na Marco Hoger wakigombea mpira Ibrahim Afellay akifanya mishe kwenye lango la ArsenalAfellay akilalamikia kukwatuliwa kwenye eneo la penalti, lakini akapewa njano akishutumiwa kujirushaFrancis Coquelakipambana na Marco Hoeger. Picha na mashirika ya Kimataifa, Reuters, AFP, Getty
Wakati huo huo, timu ya Manchester United ilichapwa mabao 3-1 na Ajax mjini Amsterdam katika mchezo wa Kundi D wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
******
Real Madrid ilikuwa nchini Ujerumani kukabiliana na Borussia Dortmund na kujikuta ikiambulia kichapo cha golei 2.1, matokeo ambayo yanaiweka Dortmund kileleni mwa kundi mbele ya timu ya Jose Mourinho. Man City wanashika mkia wakiwa na pointi moja tu baada ya kucheza mechi tatu.
Robert Lewandowski alifunga bao dakika ya 36, kabla ya Cristiano Ronaldo kusawazisha ndani ya dakika mbili, lakini Marcel Schmelzer akawafungia wenyeji la ushindi dakika ya 64.
******
Olympiacos walipata ushindi wa kwanza wakitoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Montpellier nchini Ufaransa na kuongeza ugumu katika Kundi B, baada ya Arsenal kufungwa na Schalke.
Gaetan Charbonnier aliifungia Montpellier dakika ya 49kabla ya Vassilas Torosidis kusawazisha dakika ya 73 na Kostas Mitroglou aliyetokea benchi akafunga la ushindi dakika za majeruhi.
Matokeo ya jana yanaipeleka Schalke kileleni kwa pointi zake saba, wakiizidi moja The Gunners, na Olympiacos inakwenda nafasi ya tatu na Montpellier inaburuza mkia.
*********
Malaga imeendeleza wimbi la ushindi kileleni mwa Kundi C baada ya kuifunga AC Milan 1-0 na sasa inaongoza kundi hilo kwa pointi tatu zaidi. Joaquin ndiye aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 64 kwa pasi ya Manuel Iturra.
*******
Mechi nyingine ya Kundi C, Zenit St Petersburg waliifunga 1-0 Anderlecht nchini Urusi.
Alexander Kerzhakov alifunga dakika ya 72 kwa mkwaju wa penalti, baada ya Milan Jovanovic kuchezewa rafu kwenye eneo la hatari na Alexander Anyukov.
******
Katika Kundi A, Porto imeendeleza rekodi yake nzuri ya asilimia 100 kwa ushindi wa 3-2 dhidi ya Dynamo Kiev nchini Ureno.
Wageni walisawazisha mara mbili kupitia kwa Oleg Gusev na Ideye Brown baada ya wenyeji kufunga kupitia kwa Silvestre Varela na Jackson Martinez, kabla ya Martinez kufunga la ushindi zikiwa zimesalia dakika 12.
Maelezo mengine ni kwa hisani ya AUDIFACE JACKSON BLOG
0 maoni:
Post a Comment