Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mbowe awaonya polisi

SAM_5333Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ambae pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni akizungumza kuhutubia wananchi wa Kata ya Daraja Mbili juzi katika mkutano wa kamapeni za kuwania nafasi ya udiwani wa Kata hiyo, mkutano ambao ulifanyaka katika ofisi za Kata za chama hicho.

 

****

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amelionya Jeshi la Polisi akisema haliwezi kuzima vuguvugu la mabadiliko (M4C) nchini kwa kutumia risasi kutisha na kuua wananchi.

Badala yake, amelitaka kufanya shughuli zake kwa utaalamu kwa kuzingatia sheria na kanuni zinazolisimamia na kuepuka kutumiwa kutekeleza matakwa ya watawala wanaowaagiza kuwanyanyasa wapinzani.

Mbowe alitoa onyo hilo juzi wakati akimnadi mgombea wa udiwani wa Kata ya Daraja mbili, Prosper Msofe katika Mtaa wa Jamhuri, ambaye hata hivyo hakuweza kuhudhuria mkutano huo kutokana na kulazwa Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru akipatiwa matibabu ya uti wa mgongo baada ya kushikiliwa na polisi.

Licha ya mgombea huyo kutokuwepo mkutanoni, Mbowe alimtaka kutotishika na tukio lililompata badala yake iwe changamoto ya kuzidi kudai na kupigania haki kwa maslahi ya umma.

“Kama sababu ya CHADEMA kuitwa chama cha vurugu ni kwa kutokana na hatua yetu ya kuwahamasisha watu kudai na kupigania haki zao, basi acha tuendelee kutambulika hivyo,” alisema.

Mbowe alieleza kushangazwa na hatua ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kushindwa kutangaza uchaguzi katika kata nne za Jiji la Arusha ambazo zilikuwa zinaongozwa na madiwani waliotimuliwa CHADEMA tangu mwaka jana licha ya juhudi walizofanya kuikumbusha kwa maandishi.

Kata hizo ni Elerai, Kimandolu, Kaloleni, Themi na Sombetini iliyokuwa ikishikiliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia aliyekuwa diwani wake, Alphonce Mawazo, ambaye alijivua gamba kwa kujiunga na CHADEMA.

“Woga wao wanajua nguvu ya CHADEMA kwa sasa, wanaogopa kuona tukishinda viti hivi na kuingiza madiwani sita pamoja na wa viti maalum, idadi ya madiwani wetu itakuwa kubwa, hivyo tutaongoza Halmashauri ya Jiji la Arusha,” alisema.

Akizungumzia utaratibu wa CHADEMA kuwachangisha wanachama wake fedha kwenye mikutano yao kwa ajili ya kuchangia gharama za uendeshaji, alisema kuwa chama kinajengwa na watu wenye fedha safi kama hizo.

Naye Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa wa CHADEMA, Godbless Lema, aliwataka polisi wadogo kutokubali kutumiwa kutekeleza amri za kikandamizaji za viongozi wao kuumiza wananchi kwani mwisho wa siku watakaohukumiwa ni wao.

Alisema kuwa kwenye vurugu za Arusha za Januari 5 mwaka jana, walikufa watu watatu ambapo polisi wa vyeo vya juu ndio walioongezewa vyeo huku wale wa chini wakiambulia patupu.

Source: Tanzania Daima 11 Oktoba, 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO