Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Joshua Nassari atoa siku 14 kwa magazeti mawili kumsafisha

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, ametoa siku 14 kwa magazeti mawili yatolewalo kila siku nchini kumsafisha kwa uzito waliotolea habari ya kumhusisha kufyatua risasi kwenye kata ya Daraja Mbili wakati wa uchaguzi mdogo, vinginevyo atayashitaki Baraza la Habari Tanzania (MCT).

Akizungumza na vyombo vya habari jijini hapa jana, alisema ameshangazwa kuona propaganda chafu dhidi yake zikiendeshwa kwa wazi na chuki kubwa.

“Mimi nilipita eneo la kupigia kura saa mbili kamili asubuhi nikaend kata ya ya Bang’ata wilayani Arumeru nikiwa kama wakala mkuu, kusimamia uchaguzi na tukio hili la kufyatua risasi limetokea mchana saa saba, nashangaa naandikwa mimi,” alisema.

Alisema kuwa kikubwa anachokiona ni kumpaka matope kupitia magazeti hayo.

Nassari alisema kuwa anachofahami fika magazeti hayo kupitia waandishi hao wanatumiw ana watu kumchafua kwa sababu wanazojua wao, kufuatia kushinda uchaguzi wa Jimbo la Arumeru Mashariki.

“Kwa kweli sasa sitakubaliana kamwe na tabia hii, maana nachafuliwa kwa makusudi na kusababisha wapiga kura wangu wajenge chuki dhidi yangu, alisema.

Kamanada wa Polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabasi, alipoulizwa alisema: “Mimi silijui suala hili, nimesikia katika vyombo vya habari, ninachojua mimi risasi zilifyatuliwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu, Wilaya ya Arusha (NEC), Godfrey Mwalusamba wakati akimwokoa Mussa Hamisi, aliyekatwa panga, wakati akimwokoa mama mmoja aliyedaiwa kugawa pesa za kuhonga, wapiga kura wa Daraja Mbili ili kuipigia CCM,”alisema.

Alisema Mwalusamba alilazimika kufyatua risasi baada ya kumwona Mussa Hamisi, akikatwa panga na kundi la watu hao walitawanyika na kuwa watu wanane walitiwa mbaroni.

Chanzo: Nipashe via bongonewztz

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO