Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mapato PPF yafikia bil. 91/-

MFUKO wa Pensheni (PPF) umefanikiwa kuongeza mapato yanayotokana na uwekezaji kutoka sh bilioni 43.45 mwaka 2010 hadi kufikia sh bilioni 91.38.

Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Mwenyekiti wa bodi wa mfuko huo, Dk. Adolf Mkenda, alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa 22 wa mwaka wa wanachama na wadau wa mfuko huo.

Alisema mfuko huo umeendelea kufanya vizuri, kwani katika kipindi cha Januari mpaka Juni mwaka huu mapato yatokanayo na uwekezaji yamefikia sh bilioni 47.74 ambapo imevuka malengo waliyojiwekea ya kukusanya sh bilioni 47.71 katika kipindi hicho.

Mkenda alisema PPF iliongeza fedha zilizotumika kwenye uwekezaji wa vitega uchumi mbalimbali kutoka sh bilioni 672.2 mwaka 2010 hadi kufikia sh bilioni 837.6 mwaka 2011 ambapo mfuko huo unashiriki katika ujenzi wa vyuo vikuu kikiwemo cha Teknolojia ya Sayansi ya Kompyuta kilichopo Dodoma na cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela cha jijini hapa.

Alisema PPF imefanikiwa kupata tuzo tatu tofauti kutokana na kuendesha shughuli zake kwa uwazi kwa kuzingatia utawala bora ambapo moja walipewa na Chama cha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii cha Afrika Mashariki na Kati (ECASSA) na mbili kutoka Chama cha Kimataifa cha Hifadhi ya Jamii (ISSA).

Mwenyekiti huyo wa bodi alisema licha ya mafanikio waliyopata, lakini wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za uwekezaji na kiutendaji ikiwemo kubadilika kwa riba katika amana za uwekezaji, kiwango kikubwa cha mfumuko wa bei, ufinyu wa wigo wa uwekezaji, na uwasilishwaji wa fomu za madai kutoka kwa waajiri huku wakijua wazi kuwa waajiriwa wao bado wanaendelea na kazi

Mwenyekiti wa Wakuu wa Mashirika ya Hifadhi za Jamii nchini,Daudi Msangi akitoa shukrani kwa mgeni rasmi na kwa wadau wote kwa ujumla kwa kuitika kwao wito wa Mkutano huoWakurugenzi wa Mashirika ya Hifadhi za Jamii nchi za Jirani,wakiongozwa na Bi. Magreth Osure (katikati) ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Mashirika ya Hifadhi za Jamii kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Picha ya Pamoja na Wafanyakazi wa PPF. KWA PICHA NA MATUKIO ZAIDI GONGA HAPA KUUNGANA NA BLOG YA FATHER KIDEVU

Stori imeandikwa na Grace Macha, (Tanzania Daima –Arusha); Picha na Father Kidevu

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO