Mgombea kutoka Zanzibar Khamis Sadifa Juma (pichani juu) ameibuka mshindi katika uchaguzi wa kutafuta viongozi wa UVCCM Taifa. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imekwenda kwa mwanadada Mboni Mohamed Mhita
Wajumbe wa NEC kutoka Umoja huo ni
Jerry Silaa, Deo Ndegembi, Anthony Mavunde na Jonas Nkya
WAKATI HUO HUO BASHIR NKOROMO, DODOMA ANARIPOTI KUWA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA UVCCM, MGOMBEA MMOJA ALIJITOA WAKATI WA KUOMBA KURA
Wakati ilitarajiwa kwamba uchaguzi wa kumpata Mweneyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM (Taifa) ungeweza kutoa ushindani zaidi kutokana na nafasi hiyo kuombwa na wagombea wa jinsia zote, hali ilibadilika ghafla baada ya mgombea pekee mwanamke, Lulu Abdalla Msham (pichani) kuamua kujiondoa badala ya kuomba kura.
Kufuatia kujiondoa kwake mwanamke huyo, nafasi hiyo ilibaki ikiwaniwa na madume wawili, Msaraka Rashid Simai na Khamis Sadifa Juma wote kutoka zanzibar.
Katika uchaguzi huo uliofanyika baada ya kufunguliwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere mjini Dodoma, nafasi ya Makamu Mwenyekiti wamechuana Ally Salum Hapi, Paul Christian Makonda Mboni Mohamed Mhita.
Nafasi nyingine ni, Halmashauri Kuu ya Taifa Viti sita (Bara) wagombea 40, Viti Vinne (Zanzibar) wagombea 22, Nafasi ya Baraza Kuu la Vijana Taifa Viti vitano Bara wagombea 39 na viti vitano Zanzibar wagombea 14, Uwakilishi Wazazi Taifa na Jumuia ya Wanawake Tanzania (UWT) wagombea 16 kila nafasi.
0 maoni:
Post a Comment