Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Rais Mstaafu Mwinyi apanda kizimbani

Imechapishwa Jumatano, Octoba 10, 2012 na Mtanzania

RAIS mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, jana alipanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kutoa ushahidi katika kesi yake ya kuibiwa Sh milioni 37.

Hata hivyo, wakati Rais Mwinyi akipanda kizimbani, maofisa wa Usalama wa Taifa waliwazuia waandishi wa habari wasiingie katika chumba cha mahakama alimokuwa rais huyo mstaafu akitoa ushahidi wa kesi yake.

Katika kesi hiyo ya jinai yenye namba 201, Rais Mwinyi anamshitaki aliyekuwa mfanyakazi wake, Abdallah Mzombe. Kesi hiyo iko mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Gen Dudu.

Kabla rais huyo mstaafu hajaanza kutoa ushahidi wake, alifika mapema eneo la mahakama na kupelekwa moja kwa moja katika ofisi ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Illivin Mugeta kwa ajili ya kusubiri muda wa kuanza kesi.

Wakati Mwinyi akiwa katika chumba cha Hakimu Mugeta, maofisa wa usalama wa taifa walitanda katika korido inayoelekea katika chumba hicho na kufanya kazi ya kumhoji kila anayepita eneo hilo na kuwazuia wale waliokuwa wanataka kuingia humo kwa ajili ya kupata huduma.

Ilipotimia majira ya saa tano asubuhi, walionekana askari magereza wakipita na mshitakiwa aliyefungwa pingu mikononi wakielekea katika chumba hicho cha mahakama kwa ajili ya kuendelea na kesi.

Tukio hilo liliwafanya waandishi wa habari waliokuwa wakisubiri kuingia katika chumba cha mahakama, kuinuka na kuelekea alikopelekwa mshitakiwa huyo, ambaye waliamini ndiye aliyekuwa mshitakiwa katika kesi ya Rais mstaafu Mwinyi.

Waandishi hao walipokuwa wakielekea katika chumba hicho, walizuiwa kuingia chumbani humo na maofisa usalama hao na mazungumzo kati yao yalikuwa hivi:

Ofisa Usalama: Mnakwenda wapi?

Waandishi: Mahakamani.

Ofisa Usalama: Ninyi ni akina nani?

Waandishi: Waandishi wa habari.

Ofisa Usalama: Mmeambiwa kuna mahakama humu?

Waandishi: Ndiyo kuna mahakama.

Ofisa Usalama: Tafadhalini sana haiwahusu, haiwahusu,” alisema ofisa usalama wa taifa huku mwingine akizuia waandishi kwa mikono kuingia katika chumba cha mahakama alimokuwa Rais mstaafu Mwinyi.

Kutokana na hali hiyo, waandishi wa habari hawakuweza kuingia mahakamani kwa kuwa mlango wa mahakama ulifungwa, huku Rais Mwinyi akiendelea kutoa ushahidi kwa kuongozwa na Wakili wa Serikali, Charles Anindo.

Mwinyi alimaliza kutoa ushahidi saa saba mchana na kutolewa kwa kupitia mlango wa nyuma ambako gari aina ya Land Cruiser shangingi yenye namba T 914 BJT lilikuwa likimsubiri.

Rais mstaafu Mwinyi, alitoa ushahidi katika kesi ya kutapeliwa zaidi ya Sh milioni 37 na mfanyakazi aliyemwamini kukusanya kodi katika nyumba mbili tofauti zilizopo jijini Dar es Salaam.

Katika hati ya mashitaka inadaiwa kwamba, Abdallah Mzombe, kati ya Januari 2011 na Julai 2012 maeneo ya Mikocheni, Dar es Salaam, akiwa mfanyakazi wa Ali Hassan Mwinyi, aliiba Sh milioni 17.6 alizokusanya kama kodi katika nyumba namba 481 plot A, iliyoko eneo la Mikocheni.

Fedha hizo zilikuwa ni za kodi ya mwaka 2011/2012 na 2012/2013 alizotakiwa kuzikifikisha kwa Mwinyi lakini hakufanya hivyo.

Mshitakiwa pia anadaiwa katika kipindi hicho hicho, maeneo ya Msasani Village, aliiba Sh milioni 19.8 alizokusanya kodi katika nyumba namba 55 block C iliyoko Msasani Village.

Fedha hizo zilikuwa ni za kodi ya mwaka 2011/2012 na 2012/2013. Mshitakiwa alikana mashitaka na yuko mahabusu baada ya kukosa dhamana.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO