Picha zifuatazo zinaonesha matukio tofauti katika ziara ya Diwani wa Kata ya Levolosi iliyopo Jijini Arusha, Mh Ephata Nanyaro (CHADEMA), akikagua maendeleo ya kazi ya uchimbaji kisima kwa ajili ya wananchi wa kata yake, hususani wananfunzi na walimu wa Shule ya Msingi Levolosi.
Ziara hiyo ya ukaguzi ilifanyika shuleni hapo siku ya Oktoba 10, 2012.
Diwani wa Kata ya Levolosi (mwenye nguo nyeusi), Ephata nanyaro pamoja na walimu wa Shule ya Msingi Levolosi wakiangalia namna ya uchimbaji wa kisima hicho alichoahidi wakati wa kampeni zake kuwania nafasi ya kuongoza Kata hiyo.
Mh Nanyaro (kulia) akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa uchimbaji visima ambae alieleza kuwa kisima hicho wamechimba urefu wa mita 63 kwenda chini.
Mtaalamu akielekeza matabaka tofauti ya udongo waliyokutana nayo wakati wa uchimbaji, matabaka ambayo huwasaidia kujua upatikanaji wa maji katika eneo husika.
1 maoni:
inapendeza kuona vijana wenye umri mdogo wakifanya mambo makubwa na yenye maendeleo...asilimia kubwa ya viongozi wetu wana umri mkubwa na wamekaa madarakani muda mrefu lakini hakuna chchote wanachokifanya...hongera sana kijana Diwani kwa kazi nzuri unayoifanya..natumai ni maandalizi mazuri kwa ajili ya uongozi wa juu zaidi ktk taifa letu...
Post a Comment