UCHAGUZI wa jumuiya ya umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Arusha umeingia dosari kubwa sana baada ya katibu wa CCM mkoani hapa Bi.Mary Chatanda kunusurika kichapo kutoka kwa wajumbe wa mkutano huo kwa madai kuwa wanamtuhumu kwa kumpitisha chaguo lake kitendo ambacho kiliwakera vijana hao na kusababisha vurugu kubwa katika eneo la kupigia kura
Pia Bi,Chatanda anadaiwa kuwa anatumia cheo chake kupitisha viongozi wa chaguo lake ambaye kwa jina alitajwa kuwa ni Dk.Harold Adamsom
Kutokana na vurugu hizo ambazo zilikuwa zikiendelea ililazimu zoezi hilo kuendeshwa chini ya ulinzi mkali wa polisi huku wajumbe wengine wakikataliwa kuingia ndani ya ukumbi wa kupigia kura hali iliyosababisha minong’ono ya hapa na pale
Hata hivyo Bi.Chatanda alinusurika katika vurugu hizo kutoka kwa wajumbe waliotoka Wilaya ya Monduli baada ya kuamuru zoezi la uchaguzi lirudiwe kwa madai kwamba wajumbe na wanaotoka Wilaya ya Meru idadi yao haikuwa sawa
Awali katika uchaguzi huo uliokuwa umegubikwa na na kila aina ya vijembe na vituko huku wakitambiana wenyewe kwa wenyewe huku akihusishwa aliyekuwa Waziri mkuu mstaafu aliyejiuzulu Bw.Edward Lowasa pamoja Mh.Bernad Membe
Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Uvccm mkoani Arusha kutoka wilayani Monduli wakiingia kwa mara ya pili kupiga kura za kumchagua mwenyekiti wa umoja huo baada ya zoezi la awali kuvurugika jana katika ukumbi wa CCM mkoa
Katika vurugu hizo katibu wa UVCCM Mkoa Bw. Salum kidima alitoa amri kwa waandishi wa habari kufukuzwa katika eneo hilo la jingo la CCM mkoa kwa madai kuwa haitaji waandishi wa habari
“Tokeni hapa nimesema siwahitaji hapa mkiendele kukaa hapa yatatokea makubwa kwanza hamna mashati ya kijani,,,”alisema Bw.Salum huku akifoka
Zoezi la kupiga kura za uchaguzi wa nafasi ya mwenyekiti wa Uvccm mkoa lilianza majira ya saa 6;00 mchana ambapo upepo wa awali katika uchaguzi huo ulionyesha kwenda kwa mgombea,Bw.Robinson Meitenyiku anayetokea wilayani Arusha.
Vurugu hizo zilianza majira ya saa 9;00 mchana ambapo Chatanda alipoamuru wajumbe wa mkutano huo watoke nje ya ukumbi kwa madai kwamba kuna baadhi yao kutoka wilaya za Meru na Monduli walizidi.
Kwa upande wake Elipokea Masahua ambaye ni katibu uenezi itikadi na uenezi kata ya Leguruki Wilayi Meru alisema kuwa anasikitishwa sana na kitendo cha kusimamiwa zoezi hilo na askari polisi kwani uchaguzi wa kata hadi Wilaya hawajawahi kuona askari polisi kitendo ambacho kilisababisha vijana kuona wapo chini ya ulinzi mkali hali iliyosababisha vurugu
Hata hivyo uchaguzi huo ulikuwa ukiendelea chini ya ulinzi mkali wa polisi kitendo ambacho wajumbe walionekana kupinga hatua hiyo wakidai kuwa wao sio wafungwa
Hatahivyo,mara baada ya wajumbe hao kutoka nje ya ukumbi wa uchaguzi walianza kupaza sauti kwamba katibu huyo analengo la kuvuruga uchaguzi huo kwa kuwa anataka kumpitisha mgombea wa nafasi hiyo,Dk Adamson.
Mmoja wa wajumbe hao kutoka wilayani Monduli,Bw.Isaac Kadogoo alimwakia vikali Chatanda ndani ya ukumbi huo na kumtuhumu kwamba kitendo chake cha kukaa karibu na sanduku la kura kilikuwa na lengo la kutaka kuchakachua kura hizo
Wakati hayo yakijiri nje ya ukumbi wa mkutano huo baadhi ya wajumbe walipinga kitendo cha Chatanda kuwatoa nje na kusema kwamba ana lengo la kuuvuruga uchaguzi huo ili chaguo lake lipite.
Hatahivyo,ilipotimu majira ya saa 9;15 mchana ndipo wajumbe hao walitangaziwa kurudi ndani ya ukumbi huo kwa lengo la kurudia zoezi la kupiga kura na ndipo walipojipanga kwa mistari na kuelekea katika ukumbi wa uchaguzi kupiga kura kwa mara nyingine.
Maofisa wa usalama wa taifa sanjari na askari wa jeshi la polisi mkoani Arusha walikuwa wakiranda randa nje na ndani ya ukumbi wa mkutano kuimarisha ulinzi wakiwemo na baadhi ya maofisa wa Takukuru mkoani hapa.
Kombora jingine lilirushwa kwa B.Chatanda kwa madai kuwa anaharibu chama kwa kuwa yeye ni mwajiriwa wa CCM na ndio sabau kubwa ya yeye kutaka kuendesha chama kwa matakwa yake binafsi
Hata hivyo uchaguzi huo ulirudia zaidi ya mara tatu ambapo ulimalizika majira ya saa moja usiku na kupatikana mshindi katika kinyang’anyiro hicho ambapo katibu wa chama CCM mkoa Mary Chatanda alimtangaza mshindi kuwa ni Robinson Meitenyiku aliyepata kura 247 na kumbwaga mshindani wake Dk.Harold Adamson aliyepata kura 188 huku Lightness Msemo akipata kura 4.
Soure: JAMII BLOG (PAMELLA MOLLEL)
0 maoni:
Post a Comment