Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

WATANO WAUAWA NA POLISI KILIMANJARO

Watu watano wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa katika mapambano ya kurushiana risasi katika Kijiji cha Kyara, Marangu, Mkoani Kilimanjaro leo.

Watu hao walikuwa na silaha aina ya SMG, na wanaelezwa kuwa walitoka kupora mali kwenye duka moja eneo la Marangu, na baadaye kujificha katika jumba moja eneo la Kyara ambapo walifurumushwa na Polsi na hatimaye mapambano makali ya kurushiana risasi kuanza.

Mbali na Mauaji hayo  pia askari polisi mwenye namba G.406 Pc Lameck alijeruhiwa kwa  risasi  katika mguu wa kushoto huku  walinzi watatu wakijeruhiwa kwa mapanga wakati wakijaribu kuokoa mali zilizoporwa katika duka hilo .

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Bw.Robert  Boaz amethibitisha kutokea kwa tukio hilo majira ya saa 7 usiku wa kuamkia leo baada ya kuvamia duka la Bw. Gaudence Temu na kuiba vifaa mbalimbali vya ujenzi.

Akielezea mazingira ya tukio hilo kamanda Boaz alisema kundi la majambazi watano walivamia dukani kwa Gaudence Temu na kumjeruhi kwa sime mlinzi aitwaye Hamis Juma (25) na kisha kuiba.

Alisema kufuatia tukio hilo walinzi wa sungusungu Richard Temu na Erick Yuda walijitokeza ili kutoa msaada lakini nao walishambuliwa kwa mapanga na kujeruhiwa na wote wamelazwa katika hospitali ya Kilema.

Kwa mujibu wa kamanda Boaz baada ya tukio hilo taarifa za uvamizi zilifikishwa polisi na askari wa doria walikwenda haraka eneo la tukio kutoa msaada na kuanza kuwasaka majambazi hao ambao walitokomea mara baada ya tukio hilo.

Alisema ufuatiliaji wa kina ulifanyika na kubaini maficho ya majambazi hao ambayo ni nyumba ya mmoja wao iliyopo kijiji cha Kyara eneo la Marangu, ambapo askari walikwenda na baada ya kufika waliwataka wafungue mlango na kujisalimisha lakini hawakutaka hadi Bomu la machozi lilipotupwa katika nyumba hiyo.

Alisema mara baada ya Bomu la machozi kutupwa majambazi hao walitoka nje huku wakirusha risasi ambapo chembechembe za risasi zilimjeruhi skari mmoja ambaye ni Pc Lameck kwenye mguu wa kushoto.

“Askari nao walijibu mapigo na kufanikiwa kuwapiga risasi na kuwaua majambazi watano waliojaribu kutoroka kutoka kwenye nyumba hiyo”alisema kamanda.

Aidha aliwataja majambazi hao kuwa ni Paul Baltazari Bahati (25) ambaye ni mwenye nyumba, Remius Msambure kwa jina maarufu mreno (30) ,Focus Daud Mtui ( kwa jina maarufu Kisinja (35) wote wakazi w kijiji cha Kitowo Marangu,Elia aliyetambulika kwa jina moja mmasai mkazi wa kijiji cha Msitu wa Tembo na mmoja bado hajatambulika.

Kamanda alisema katika eneo la tukio ilikutwa bunduki moja aina ya Shortgun greener yenye No. 858356 na risasi nne, maganda ya risasi ambapo bunduki hiyo iliibwa Tarehe septemba 15 mwaka huu katika kijiji cha Chemchem wilaya ya Moshi kwa Bw. Kribia Bwanakule Mmari.

Vingine ni Pistol aina ya Browning ambayo imefutwa namba na risasi mbili,Risasi 10 za bunduki aina ya SMG,Mapanga,sime,yenye damu, Brief case yenye mabomba ya sindano,sindano, uzi wa kushonea majeraha hospitali,zana mbalimbali za kuvunjia pamoja na mali mbalimbali za wizi.

Hata hivyo baadhi ya wakazi wa moshi wamepongeza hatua ya jeshi hilo na kusema kuwa majambazi hao wamekuwa kero katika kijiji hicho kwa muda mrefu hali ambayo ilikuwa ikiwanyima usingizi kwa kuhofia kuvamiwa

Source: Kamanda wa Matukio, Richard Mwaikenda na DJ Sek Blog

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO