Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Tigo, American Garden walivyowa-surprise watoto katika ‘Happy Birthday’ ya Andrew Chale

KAMPUNI ya Tigo Tanzania leo Oktoba 21, imeweza kufanya ‘surprise’ mbalimbali kwa watoto waliojitokeza katika siku maalum ya kuzaliwa kwa mdau na mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima na blog, Andrew Chale, iliyofanyika ndani ya viunga vya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es Salaam.

Katika party hiyo maalum, Andrew Chale amesema ni ya kwanza kabisa kwa Mtanzania kufanya hivyo kwani ilianza tokea           Oktoba Mosi  kwa kutembelea vituo vya watoto waishio kwenye mazingira magumu na hatarishi  na kutoa misaada na pia kutembelea watoto mahospitalinio na kuwafariji.

Akielezea mtandao huu, Andrew Chale anasema alimwamini Mungu muda wote ndio maana ameweza kufika hapo na pia kutumia nafasi hiyo kwa pamoja kufurahi na watoto hao wakiwemo wale waishio kwenye mazingira magumu.

“Leo, ni siku muhimu sana kwangu, najiona nipo na mamilioni ya marafiki kwa kufika kwenu kumenitia sana faraja Mungu awabariki nyote” alisema Andrew  wakati akiwashukuru watoto mbalimbali waliojitokeza kufanya nao sherehe hiyo.

Watoto hao wakiwemo waliotoka kwenye vituo vya kulelea watoto vikiwemo vya  Tanzania Mitindo House kilicho chini ya Mbunifu,Khadija Mwanamboka, New Life Orphanage center  cha Kigogo, watoto waishio mitahani na wale wa majumbani walijumuika kwa pamoja na kufurahia na ‘Uncle’ wao Andrew Chale  ikiwemo kutembelea sehemu kadhaa za ndani ya jumba hilo la kumbukumbu na kujionea mambo mbalimbali.

Furaha hiyo ya siku maalum ya kuzaliwa kwa Andrew Chale imeweza kuongezwa utamu na kampuni ya Mawasiliano ya mtandao wa simu nchin, Tigo Tanzania, ambayo iliwezesha kumpatia keki na shampeni  maalum pamoja na zawadi zingine nyingi kwa watoto.

Kwa upande wake Ofisa wa masoko wa tigo, Benny  Lutaba, alipongeza kwa sherehe hiyo na kuomba jamii kuendelea kuwaunga mkono kwa bidhaa zao hapa nchini sambamba na kusaidia jamii kwa rika zote.

Nae Wenceslaus Kisarika ambae ni Marketing Manager wa K&K pamoja  Cons  Ltd  alipongeza kwa hatua ya watu kukumbuka watoto hasa waishio kwenye mazingira hatarishi na magumu hapa nchini.

“Tumefarijika sana kuunga kwenye siku hii muhimu, hakika jamii iiige mfano huu wa kuwakumbuka watoto hasa wanaohitaji msaada si utoe fedha hata kuwaleta mahala kama hapa ni moja ya kuwatimizia mahitaji yao” alisema Wence.

Aidham mbali na tigo,  American Garden kwa upande wao waliweza kuwa ‘surprise’ watoto  kwa kuwapatia zawadi za bidhaa zao zinazopatikana nchini kote.

Akizungumza na mtandao huu kwenye sherehe hiyo, Ofisa masoko wa Kingsway International (T) ltd,  American Garden, Miraji Chambuso  alipongeza kwa hatua hiyo ya kuwakumbuka watoto hao na ni moja ya kuhamasisha utalii wa ndani.

“Watoto wanapopata nafasi ya kufika sehemu kama hizi ni kuhasisha utalii wa ndani na sisi tupo mstari wa mbele katika kuhakikisha watoto wanatimiza ndoto na malengo yao” alisema Miraji. Picha na Andrew Chale kwa msaada wa FATHER KIDEVU

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO