na Grace Macha, Arusha
KAMBI ya Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, imeendelea kuibuka na ushindi kwenye chaguzi mbalimbali zinazoendelea ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya Flora Zolote kuibuka mshindi kwenye kinyang’anyiro cha uenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) wa mkoani Arusha.
Katika uchaguzi huo uliofanyika juzi katika Kituo cha Mikutano cha Arusha (AICC) aliyekuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Nembris Kimbele, aliyekuwa anaungwa mkono na katibu wa CCM mkoani hapa, Mary Chatanda, alibwagwa vibaya baada ya kuambulia kura 201 dhidi ya 254 za Zolote ambapo kura moja iliharibika.
Matokeo hayo yalitangazwa na Chatanda ambaye ndiye alikuwa akisimama pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela, ambapo Katibu Mkuu wa zamani wa UWT, Halima Mamuya, alichaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza Kuu Taifa; na Lucy Bongele alichaguliwa kuwakilisha mkutano wa wazazi.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Arusha, Namelok Sokoine, akichaguliwa kuwakilisha jumuiya hiyo katika mkutano wa vijana (UVCCM) huku mweka hazina mstaafu wa CCM taifa, Sifa Swai, akichaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la UWT Mkoa pamoja na Jesca Mboga huku Tina Timan akichaguliwa kuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu UWT Taifa
0 maoni:
Post a Comment