Mgombea udiwani Kata ya Daraja Mbili Arusha ku[pitia Chadema, Propser Msofe akiwa zahanati ya Polisi Arusha mapema leo asubuhi baada ya hali yake kuonekana sio nzuri.
Msofe alikamatwa jana usiku na kulazwa mahabusu ya Polisi Makao Makuu Arusha na kuandikiwa shitaka la kufanya shambulizi la mwili kwa mtu mmoja aliedai kupigwa nae jana usiku maeneo ya Friends Corner.
Hata hivyo mtu huyo anaelezwa kuwa ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na amekuwa ni mtu mwenye rekodi ya msuguano na wanasiasa wengi ambao huwatambia kwa kuwafikisha Polisi. Ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Raha Promotion, maarufu kama Rama, kampuni ambayo ina tenda ya kufanya matangazo ya manispaa ya Arusha na kwa muda mrefu kampuni hiyo imekuwa ikilalamikiwa sana kuwanyanyasa wananchi hasa wafanyabiashara ndogondogo kwa kuingilia kazi ambazo sio halali yao.
Kwa mujibu wa taarifa ya kisa kizima cha kuakamtwa Msofe hadi kuwekwa ndani, inaelezwa kuwa Msofe alikuwa anatoka kuwafikisha nyumbani baadhi ya watu waliokuwa kwenye kikao nyumbani kwake hadi saa mbili kasoro usiku akitumia gari yake ndogo. Wakati anarudi ndipo akakutana na wamama wafanya biashara za mboga mboga wanapigwa usiku huo na huyo mtu wa Promotion na vijana wake ndipo akaamua kuhoji kinachoendelea.. Kilichofuata ni kushushiwa kipigo na baadae kupelekwa polisi na kufunguliwa shauri hilo.
Hapa yupo ndani ya gari ya Polisi akipelekwa Mahakama ya Mwanzo Maromboso iliyopo Levolosi baada ya kuonekana akiendelea kusubiri kituoni pale watu wengi wangejaa na kuzuia shughuli nyingine.
Mh Godbless Lema akiteta jambo na Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha nje ya viwanja vya Polisi Makao Makuu Arusha
Baadhi ya viongozi na wanachama wa Chadema waliojitokeza viwanja vya Mahakama ya Mwanzo Maromboso mapema leo asubuhi wakishauriana mambo kujua hatma ya mgombea wao.
Kundi la waandishi wa habari waliojitokeza Mahakamani hapo kufuatilia sakata hilo la mgombea wa Chadema Kata ya Daraja Mbili
Baadhi ya wananchi waliojitokeza viwanja vya Mahakama
Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha, Bw Sarungi akizungumza na afisa wa Polisi, kwa nyuma Msofe anaonekana akiliendea gari la Polisi kuingia ndani.
Prosper Msofe akidandia karandika ya Polisi kuelekea Mahakamani mapema asubuhi leo
Hapa Msofe anapelekwa wodini kulazwa baada ya kuchekiwa afya yake. Mwenyewe alidai alipigwa akiwa mahabusu
Mgombea wa Chadema akiwa amepumzishwa kitandani katika wodi ya majeruhi Hospitali ya Mt Meru Arusha..
0 maoni:
Post a Comment