Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: RICK ROSS KATIKA SHOO YA SERENGETI FIESTA DAR 2012 JANA

Mtu mzima Rick Ross “The Boss” kutoka nchini Marekani akiwa jukwaani kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linalofanyika kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar salaam ,alikamua ile mbaya na mashabiki wakapagawa vyakutosha kwa kila anachowaelekeza kufuata wanafuata jamaa amefunika mbaya, hiii ni mara yake ya kwanza kufanya onesho nchini Tanzania

Rick Ross akipagawisha mashabiki wake usiku wa jana kwenye viwanja vya Leaders.

Sasa ni zamu ya Lina wa THT akiwa jukwaani akiimba wimbo wake wa nampenda ambao umewafanya mashabiki wa muziki kuitikia kwa nguvu wakati akiwaimbisha hapa akipozi kwa staili ya aina yake huku akiwaimbisha mashabiki wake

Rick Ross hapa akiwaelekeza jambo mashabiki hawapo pichani wakati alipokuwa akiimba jukwaani usiku wa jana

Rachel na wacheza shoo wake wakiburudisha mashabiki viwanja vya Leaders jijini Dar es salaal katika tamasha la Serengeti,

Watu wa usalama wakijaribu kudhibiti rapsha zilizokuwa zikijitokeza  kutokana na mashabiki wengi kuwa na hamu ya kumuona mwanamuziki Rick Ross.

GARI ALILOKUJA NALO RICK ROSS BONGO

Hayo ndio yalijiri usiku wa jana katika shoo ya rick rose mnyamwezi.

SOURCE: GLOBAL PUBLISHERS LTD

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO