Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

UZINDUZI WA KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA DARAJA MBILI ARUSHA KAMA KAMPENI YA URAIS

Jana Jumamosi Oktoba 6, 2012 katika eneo la Ndarvoi, kata ya daraja Mbili kulifanyika mkutano mkubwa wa hdahara ambapo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilikuwa kikizindua rasmi kampeni za kuwania kiti cha udiwani katika Kata hiyo.

Wananchi wengi sana walijitokeza eno hilo kusikiliza hotuba za viongozi wa Chadema walippangwa kuhutubia na kumfahamu mgombea wa Chama hicho na sera zake. Umati wa watu ulikuwa mkubwa kiasi cha kufanania baadhi ya mikutano ya chama hicho iliyowahi kufanyika kwa ngazi ya urais au ubunge.

Baadhi ya watu waliozungumza katika Mkutano huo ni Godbless Lema aliekuwa mzungumzaji mkuu sambamba na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Mh Joshua Nassari ambao kwa pamoja walikong anyoyo za watu kiasi cha kushangiliwa kila mara.

Wengine ni aliewahi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Arusha, James Ole Millya, Diwani wa Kata ya Levolosi, Mh Ephata Nanyaro, madiwani wengine wa chama hicho Arusha pamoja na mgombea mwenyewe, Ndg Prosper Msofe.

Awali kulikuwa na taarifa za Dr Slaa kuhudhuria uzinduzi huo lakini ikataarifiwa baadae kuwa alipata udhuru na kushindwa kuhudhuria. Taarifa zinaeleza kuwa Katibu Mkuu huyo pamoja na mwenyekiti Mbowe, jana walikuwa Wilayani Rombo kwenye shughuli ya uzinduzi na leo wanatarajiwa kuwa maeneo ya Vunjo Moshi.

Tukio jingine ambalo lilisisimua wananchi waliohudhuria lilimhusu mzee mmoja aliehama CCM rasmi jana hiyo na kukabidhiwa kadi ya uanachama wa Chadema na Mh Lema.

Mzee huyo, maarufu kama Mzee Zakaria anaelezwa kuwa alikuwa mtu muhimu sana kwa CCM katika Kata hiyo. Alipopewa nafasi ya kusalimia wananchi alitumia sehemu kubwa ya mazungumzo yake kuchambua madhaifu ya chama hicho katika miaka 50 ya kujitawala na kudai kwamba kwa muda wote huo nchi imedumaa.

Mzee Zakaria akasema anashangaa Serikali ya CCM inapodai inapambana na ujinga wakati haitaki kusikiliza na kutatua malalmiko ya walimu, watu ambao alidai ni muhimu kwa taifa lolote. Alizungumzia ugumu wa maisha na kutolea mfano wa usafiri wa treni kwamba kama ungeboreshwa usafirishaji wa bidhaa ungekuwa rahisi na gharama za bidhaa zisingekuwa za juu sana, na mwisho akadai kuwa CCM itatolewa madarakani na Mungu kwa maovu wanayowatendea wananchi na sio Chadema.

DSCN5626Aliekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (mwenyewe anasema yupo likizo) baada ya ubunge wake kutenguliwa na Mahakama akimnadi mgombea wa chama chake Ndg Prosper Msofe, kwa maandalizi ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hapo baadae kumpata Diwani wa Kata hiyo jana.

DSCN5609Mbunge wa Arumeru Mashariki, Mh Joshua Nassari (CHADEMA) akihutubia katika mkutano wa jana. Pamoja na mambo mengine alizungumzia na kulaani tukio la kutoroka kwa watuhumiwa wawili wa mauaji ya aliekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Kata ya Usa-River, Arumeru. Nassari alisema kwamba juzi akiwa Simanjiro alitaarifiwa kutokea kwa tukio hilo Mahakama Kuu Arusha kwamba watuhumiwa wawili kati ya sita wametoroka wakiwa chini ya ulinzi wa Polisi wenye silaha.

Mh Nassari alienda mbali zaidi na kusimulia kisa cha Mwenyekiti huyo kuuwawa kikatili kwa kuchinjwa shingo na msumeno kuwa ni kutokana na kutoa siri ya mazungumzo na mbunge mmoja wa chama pinzani na chake ambae hakumtaja jina, aliyetaka kumuhonga ili avujishe siri za Chadema wakati ule wa kampeni ya Arumeru Mashariki ambapo Nassari aliibuka kidedea.

Mh Nassari alirudia tena kuitahadharisha Serikali na Jeshi la Polisi kuwa kama wauaji wasipopatikana kwenye mikono ya Polisi hali itakuwa tete Mkoani Arusha.

DSCN5620Lema akitambulishwa na Mh Nassari na kupewa sifa lukuki na mbunge huyo kwa namna anavyopambana na misukosuko ianyompata katika kupigania haki za watanzania na chama chake bila kuchoka.

DSCN5597James Ole Millya katika benchi na viongozi wengine hiyo jana. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Vijana Wilaya ya Arusha (CHADEMA), Noel Olevaroya. Anaemfuatia kutokea kushoto kwake ni mgombea wa Chadema, Msofe na Mh Lema

DSCN5610Wananchi wakinyoosha mikono kuitikia miongozo ya Mh Nassari ambae haonekani pichani

SAM_4965

DSCN5636Mh Lema akielezea kwa ishara namna Msafiri Mbwambo alivyochinjwa kwa msumeno na baadae watuhumiwa wa mauaji hayo kudaiwa kutoroka mikononi mwa Polisi.

Katika mkutano huo Godbless Lema alizungumzia mambo mengi baadhi yake ikiwa ni kuhusu umuhimu cha chama chake kuhsinda uchaguzi wa Kata ya Daraja mbili, propaganda za udini na ukabila, na swala la wafanyabiashara ndogondogo Mkoani Arusha.

Lema alisema uchaguzi wa Kata ya Daraja Mbili chma chake hakiuchukulii kama uchaguzi wa Kata tu. Ni uchaguzi ambao utatoa muelekeo wa siasa ya chama chake nchini na hususani mkoani Arusha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Akasema kuwa Operesheni ya M4C imeahirishwa kwa muda ili kusaidia kampeni za Kata zinazoendelea nchini kote na kudai kwamba makamanda wa chama hicho wamejigawa kwa kanda tofauti. Yeye Lema na Nassari watakuwa mikoa ya Kaskazini, Mwenyekiti Mbowe anasimamia Mikoa ya Kusini.

James Ole Millya na banaga watakuwa wakiongeza nguvu mikoa ya Dodoma na Morogoro wakati Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dr Slaa amekabidhiwa mikoa ya Kanda ya ziwa.

Kuhusu propaganda za udini na ukabila, Lema alisema propaganda hizo zimefanywa na CCM na Serikali yake kwa muda mrefu na kwamba zikiachwa ziendelee zitalipeleka taifa mahali pabaya. Akatolea mfano wa Chama Cha Wananchi CUF (bila kukitaja jina) kuwa kiliruhusu propaganda hizo ziwamalize lakini Chadema wameligundua mapema na hawataruhusu kuhujumiwa na propaganda hizo alizodai hazina nia njema na taifa. Alikumbushia kuwa CCM ilikuwa mstari wa mbele kuitangaza CUF kuwa ni chama cha kiislamu na tukio la aliewahikuwa IGP, Omar Mahita kuonesha majambia na kudai yaliletwa na CUF kwa ajili ya vurugu. Alimtaka Rais Kikwete na vyama vingine vya siasa kuchagua viongozi wake kwa kuangalia utendaji wao na sio dini au kabila zao.

Swala la mgogoro wa machinga na Manispaa ya Arusha nalo lilizungumzwa mabpo Lema alisema sio haki kutumia bunduki kuwatoa watu mjini. Alidai kuwa kuwepo kwa machinga wengi ni matokeo ya Serikali ya CCM kushindwa kuongoza nchi vizuri.

Akisisitiza zaidi, Lema alisema kuondoa machinga mijini sio lazima kuwafukuza kwasababu wapo mjini na kufanya umachinga kwa vile hawana ajira. Lema alisema kuwa viwanda vilivyokufa kwa ufisadi vingeweza kutoa ajira kwa vijana na tatizo la wamachinga lingekuwa na suluhisho.

Akimnadi mgombea wa Kata hiyo kupitia Chama chake, Prosper Msofe, Mh Lema alimhakikishia kuwa kwa mapokezi waliyoyapata jana katika siku ya uzinduzi ni wazi kuwa tayari Kata hiyo imeenda chadema hata kabla ya uchaguzi, kwa kununuu msemo wa Mbunge wa iringa Mjini (CHADEMA) Mch Peter Msigwa kuwa “wali wa kushiba unauona kwenye sahani”

Lema alimtaahadharisha mgombea wake kuwa chama chake hakilei watovu wa nidhamu na wasio waadilifu na kudai kwamba hata yeye akija kuonekana hana uadilifu katika kuwatumikia wananchi, chma hakitasita kumuondoa kama ilivyowahi kutokea kwa madiwani wa Arusha na Mwanza. Alidai kuwa lengo la Chadema sio kushika madaraka bila uadilifu.

“Tutaendelea kufukuza mamluki na wapambe wote ili tukipewa mamlaka ya taifa hili tulipeleke mahali pazuri” alisema Lema.

Mh Lema aligusia pia uwepo wa taarifa kuwa kuna zaidi ya sh milioni 500 zimetengwa na chama ambacho hakukitaja kwa ajili ya kuhonga wananchi wa daraja mbili. Lema akawaambia pesa hizo zikija wasiache kuzichukua.

DSCN5648

DSCN5676Mh Godbless Lema akimkabidhi kadi ya uanachama Mzee Zakaria baada ya kumvalisha skafu na kofia zenye rangi za Chadema, mwananchama mpya wa chama hicho alietoka CCM. Wanaoshuhudia ni Diwani wa Levolosi ambae pia ni Mwenyekiti wa Vijana Mka wa Arusha, Ephata Nanyaro na mgombea wa chama katika Kata hiyo, Prosper Msofe.

SAM_4989Mzee Zakaria akizungumza kuwasalimia wananchi. Mkononi ameshika barua ambayo alidai ameandikiwa na CCM wakimtaka asiondoke.

SAM_4988

DSCN5596Ephata Nanyaro akiwajibika jukwaaani

DSCN5632“VUA UKANDA VAA UKAMANDA”

SAM_4943

DSCN5693Lema akiwa na mgombea wa chama chake wanaondoka eneo la mkutano hadi nyumbani kwa mgombea.

DSCN5687Wananchi wakiwa wamejpanga njiani kumlaki Lema na mgombea wa chama chake na kisha kusindikiza msafara hadi nyumbani kwa mgombea.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO