Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Taswira: Matukio Zaidi Katika Eneo Ambapo Wachimbaji Zaidi ya 15 Waliofukiwa Na Kifusi Cha Moram Jijini Arusha Jana; Majina ya Marehemu haya Hapa!

Kufuatia kuporomoka kwa gema la mwamba jana na kufukia wachimbaji wanaokadiriwa kufikia 18 Jijini Arusha, katika machimbo ya moram yaliyoko eneo la Moshono, Mkuu wa Mkoa, Magessa Mulongo aliagiza machimbo yote ya mchanga kufungwa hadi hapo serikali itakapotoa amri ya kuendelea na shughuli za uchimbaji

Tukio kama hili liliwahi kutokea mwaka 1997 ambapo watu 7 walipoteza maisha na uongozi wa Jiji uliwaagiza wachimbaji kutumia katapila badala ya mikono, jambo ambalo halikutekelezwa ipaswavyo.

Hata hivyo  wananchi waliishutumu vikali serikali kwa kushindwa kuboresha miundo mbinu ya eneo hilo kwa kuwa tukio kama hilo si mara ya kwanza kutokea hivyo walidai kuwa ni uzembe wa hali ya juu

Hadi kufikia jana jioni, maiti za watu 13 ndiyo zilikuwa zimeopoelewa wakati watu wawili tu ndiyo walikuwa wametoka wakiwa hai na kukimbizwa katika Hospitali ya Mt Meru kwa ajili ya matibabu kutokana na kuvunjika miguu.

Waliotolewa wakiwa hai walitambuliwa kuwa ni Matei Nenano na Lushooki Laizer wote wakazi wa jijini Arusha.

Maiti zilizoopolewa ni za mmiliki wa magari ya kubeba kifusi hicho, Julius Peter, Alex Mariaki, Gerald Lutakata, Hassan Hamis, Sauli Raphael, Bariki Revelian na Kababuu Ruafela.
Wengine ni Mwenda Kiboliboli, Japhet Jivaline, Benard Masai, Gerald Jacob, Fredy Losileani, Julius Palangyo na mtu ambaye alijulikana kwa jina moja la Christopher.

Watu walioshuhudia tukio wanasema ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 5.00 asubuhi wakati shughuli za uchimbaji zikiendelea huku mvua inanyesha, na ndipo ghafla gema la mwamba liliporomoka na kuwafunika.

Taarifa mpya kwa leo zinaeleza kwamba zoezi la utambuzi wa miili ya marehemu unatarajiwa kufanyika leo katika Hospitali ya Mt Meru.

IMG_0646
Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Mh Joshua Nassari, wote kutoka CHADEMA wakisaidiana na askari jeshi kufanya uokozi wa miili ya marehemu jana mchana.

IMG_0639

IMG_0640mmoja wa miili ya marehemu ikitolewa kwenye kifusi

IMG_0632Mh Lema akihojiwa na waandishi wa habari katika eneo la ajali

IMG_0645

IMG_0648Kichwa cha Scania tani 18 kikianza kuonekana baada ya kufukuliwa

IMG_0643

IMG_0644Wabunge wa Chadema, Arusha Mjini na Arumeru Mashariki wakifuatilia tukio la uokozi

IMG_0637

IMG_0629

IMG_0650Scania kama linavyoonekana baada ya kufukuliwa

Picha zote na Arusha255 Blog “Noize of Silence”

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 maoni:

Unknown said...

Poleni sana ndugu zetu wa Arusha roho zinauma sana kwa matukio kama haya lakini tufanyaje????????? Kazi ya mola haina makosa......muangu ilaze mahali pema peponi roho za marehemu..........tupo pamoja ktk wakati huu mgumu.........amen

Unknown said...

Poleni kwa yaliyowakuta ila tuzidi kumwomba mwenyezi Mungu atuepushie matatizo kama hayo,,, Amen

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO