Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Dr Slaa kuzindua kamapeni za Udiwani Kata ya Daraja Mbili Arusha kesho

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anatarajiwa kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika jiji la Arusha kesho Jumamosi Oktoba 6, 2012 kuanzia saa 8 mchana katika uwanja wa Ndarvoi, Kata ya daraja Mbili jijini hapa.

Mkutano huo utaenda sambamba na uzinduzi rasmi wa kampeni za Udiwani katika Kata hiyo.

Tayari kuna hekaheka kubwa katika jiji la Arusha kuhusiana na mkutano huo ambapo mazungumzo ya watu mbalimbali yanazungumzia mkutano huo.

Mkutano huo unafanyika ikiwa ni takribani wiki moja tu imepita tangu chama  cha CUF kilifanya mkutano wake mjini hapa na kuhutuiwa na viongozi wake wote wa kitaifa. Hata hivyo, katika kile kinachohisiwa ni kuhofia kukusa watu wa kuwahutubia, chama hicho kililazimika kusafirisha watu zaidi ya 400 kutoka mikaoa ya Dar-es-Salaam, Morogoro na Tanga na  kwenda kuwahutubia Arusha.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO