Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Watuhumiwa wa mauaji ya aliekuwa Mwenyekiti wa Chadema Usa-River wametoroka Mahakamani chini ya ulinzi wa Polisi

Watuhumiwa wawili kati ya watatu wa mauaiji ya aliekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Usa River, Arumeru, Bw Msafiri Mbwambo, wametoroka Mahakamani wakiwa chini ya ulinzi wa polisi jana.

Watuhumiwa hao walikamatwa hivi karibuni wakiwa mafichoni Wilayani Kondoa baada ya kuuawa kwa Mwenyekiti huyo siku chache baada ya kukamilika kwa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki ambapo aliekuwa mgombea wa CHADEMA, Joshua Nassari aliibuka mshindi.

Watuhumiwa hao walitoroka mchana jana walipokuwa katika viwanja vya Mahakama Kuu Arusha.

Ilielezwa kuwa moja wa watuhumiwa hao, alimvamia mmoja wa askari waliokuwa wanalinda watuhumiwa Mahakamani hapo na kumnyang’anya bunduki aina ya SMG na kuanza kutishia Polisi kisha kukimbia na mtuhumiwa mwenzake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas licha ya kupigiwa simu yake mara kadhaa kuelezea tukio hilo, hakupokea na baadae mmoja wa maofisa wa Polisi licha ya kuthibitisha tukio hilo, alisema isingekuwa rahisi kuonana na kamanda huyo jana.

“Unajua mimi si msemaji wa Polisi ila tumepata taarifa hizi na bunduki iliyoporwa imeokotwa, ila kamanda yupo katika mapokezi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema” alisema.

Alisema kiongozi wa Polisi ambae alikuwa Mahakamani aliyemtaja kwa jina moja la Meja Mohamed alikamatwa na hadi jana alikuwa mahabusu.

Mara baada ya tukio hilo, wananchi mbalimbali wa Jiji la Arusha walipashana ujumbe wa simu na kusababisha tukio hilo kuwa gumzo kubwa.

Mmoja wa waliopokea ujumbe huo, aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema alisema taarifa hiyo imeshitua.

Published by Mwananchi, 5 October, 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO