Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Exclusive Interview ya Mh Lema na Milard Ayo wa millardayo.com

 

Kwenye Exclusive interview aliyofanya na millardayo.com, Godbless Lema (Chadema) alievuliwa ubunge wa Arusha Mjini na Mahakama amezungumzia kuhusu vitu ambavyo chama cha Mapinduzi (CCM) kinakosea.

Anaanza kukaririwa akisema “kwanza ni uaminifu, vilevile ukishaona chama viongozi wake wanakosa vision kwa sababu hata katika maisha ya kawaida unafikia malengo kama una maono, muulize Waziri yeyote wa CCM ama kiongozi yeyote wa CCM, maono yao ya msingi ni ya kuweka CCM madarakani kwa gharama yoyote”

“Wajenge shule na waweke walimu wazuri ziwe na hadhi kama hizi English medium, wanasema wamefanikiwa wamejenga shule za kata, nionyeshe mtoto wa waziri mmoja anaesoma shule ya kata… jambo la msingi ambalo CCM wamelikosea sana ni kukosa vision, hakijui kinataka kuacomplish nini, kwa sababu kimekosa vision.. kimekosa teamwork yenye lengo moja, teamwork ya CCM ridhaa yao ni kushika power na sio kujenga maisha ya watu” – Lema

Alipoulizwa kuwa ni kiongozi gani wa CCM anaedhani ni mwema na anafaa kuhamia Chadema……. akajibu “wako watu, sio watu wote wabaya.. wako watu wanafiki, wezi na mafisadi, ushauri wangu kwa hao wazuri wanaofikiri wao wana wema wa kutosha wana nia nzuri na nchi yao, hii ni moment sasa ya kuja kuungana na jeshi lakini sio kama akina Sitta, hao wabaya ambao kwanza hata wakija hatuwapokei wasubiri jela tutakapochukua nchi, kuna watu watakwenda jela.. yani uzee wao kuna watu watastaafia jela kwa sababu wameifilisi nchi, CCM haiwezi kuwa na watu wote wabaya… wako wadogo wazuri lakini hao wakubwa hapo juu ndio wana shida”

Chanzo: MILLARD AYO

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO