Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Taswira Mbalimbali Za Mkutano Wa CHADEMA- Iringa

Chama cha demokrasia na maendeleo chadema leo kimefanya mkutano wa hadhara ambao ulihudhuliwa na mamia ya watu.
Viongozi kadhaa wa chama walikuwepo miongoni mwao ni Mh.Nassari,Mh.Msigwa na kamanda Bananga ambae amejiunga na CDM akitokea CCm yapata miezi mitano iliyopita.
Mambo mengi yamezungumzwa na viongozi hawa walipokuwa wakihutubia Manispaa ya Iringa katika eneo la Mwembetogwa ambapo ndipo mkutano umefanyika.
Viongozi hawa wa CDM wamewataka wana Iringa kutodanganywa na wanaopita mitaani kukitukana chama na kumkashifu Mh.Msigwa
Pia wamelaani vikali mauaji ya muandishi wa habari Daud Mwangosi na wamemshangaa Mh.Rais kwa kushindwa kutoa hata rambirambi kama alivyofanya kwa marehemu Kanumba!Viongozi hawa wamewataka wananchi kutohofia kufa ili ukombozi wa kweli katika nchi hii uweze kupatikana

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO