Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MWALIKO WA MWANDISHI ANDREW CHALE KUTEMBELEA VITUO VYA YATIMA NA WAZEE KATIKA WIKI YA KUADHIMISHA KUZALIWA KWAKE

andrew chaleHello Friendz;

Katika kuelekea siku yangu ya kuzaliwa, yaani October 21, natarajia kufanya yafuatayo.

(1) October 6,nitatembelea moja ya kituo cha kulelea watoto na kuwafariji.

(2) October 7,nitatembelea kambi ya wazee huko Kigamboni na kuwafariji

(3) Otober 13,nitapata wasaha wa kukaa na watoto wa mtaani wa maeneo mbalimbali waliopo katikati ya jiji, hii ikiwemo kuwa nao kwa muda wa siku nzima, ikiwemo maeneo ya Posta,Kariakoo, gerezani,Jangwani na ferri (Hii ni kwa maeneo yote wanapopatikana waoto hawa.

(4) October 14, nitakuwa kwenye fukwe za Kigamboni, na marafiki ambapo pia watakaojumuika siku hiyo watapata kufundishwa namna ya kuogelea kwenye maji, sambamba na kujiokoa endapo itatokea matatizo.

(5) October October 20,nitatembelea Ocean Road kwenye wodi ya watoto na baadae nitaelekea Muhimbili kwenye wodi ya watoto na wamama wamama.

…October 21 nitaelekea kanisani na baada ya hapo ni kufurahia kwa pamoja na marafiki./

Ukiwa miongoni mwa #TEAM ANDREW CHALE# unakaribishwa sana usisite, kwani Andrew Chale, katika maisha yake hapa duniani anakutegemea wewe na ameishi miaka yote tokea saa 12,jioni, October 21,1985, alipozaliwa pale Muhimbili Hospital, mpaka leo hii amekuwa na kufikia hapa ameishi na wewe.

Kwa pamoja, Andrew Chale ambaye awali aliishi katika maisha ya taabu ikiwemo ya watoto wa Mtaani, na baadae kuachana na maisha hayo (Street children-3yrs) na baadae kuja kuishi na watu baki (2yrs) na maisha ya kujitegemea (7yrs) mpaka sasa muda huu.

Hakika kwa neema zake Muumba sina la kumrudishia zaidi ni asante, kwani licha ya kuwa na shida na taabu kila kukicha najikuta maisha yangu yanaongezeka mbali ya kutokuwa na kazi ambayo nalipwa mshahara, lakini nakula, kunywa,nalala,natembea nacheka na hakika wapo watu hapo hapo ambao wanalipwa mshahara na malupulupu hawaishi kwa raha wanaomba ni bora wafe…kwa mimi nasema ASANTE MUUMBA.

Hivyo kwa kuipenda nchi yangu na kuwasaidia vijana wenzangu na watoto wa nchi hii, nimefanikiwa kuanzisha taasisi mbili ikiwemo ile ya ; Magomeni Youth Development Group-ama MAYODE, Ambayo lengo kubwa ni kuakikisha vijana wa Magomeni wanafika mbali kwa kujishughulisha ikiwemo kufanya kazi za kujipatia kipato.

Kwa taasisi ya Mayode Group iliniwezesha kupata mfadhiri, Sir Rita Tolant, (mother), na aliweza nisomesha elimu yote ikiwemo uandishi wa Habari na kozi zingine, nitamkumbuka daima coz aliweza fungua mwanga wa maisha yangu mpaka kufikia hapa.

Katika kuona watoto wengine wanatoka kwenye manyanyaso yakiwemo ya kutekwa na kufanyiwa vibaya na watu wasio wema huko mitaani na watoto kutumikishwa, nilianzisha taasisi ya ‘HAKIMTOTO FOUNDATIO’ ambayo kazi kubwa ni kutetea watoto.

Kwa pamoja na atakeguswa na hili nyote munakaribishwa kwenye moja ya shughuli hizi muhimu ambayo itaanza mwishoni mwa wiki.

KAMA UNACHOCHOTE KITU CHA KUTOA KWA AJIRI YA WENGINE UNAKARIBISHWA NA PIA KAMA UPO MBALI UNAWEZA KUWASILIANA NAMI AMA KUMTUMA MWAKILISHI.

Wasiliana name 0719076376 au 076707637..ASANTE.

Andrew Chale

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO