Hapo awali ilielezwa kuwa wakati Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikisitiza kufanya maandamano leo kisha mkutano mkubwa wa hadhara, kuliibuka mvutano baina yake na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, kufuatia Kamanda wake, Faustine Shilogile kupiga marufuku mandamano hayo.
Kamanda Shilogile alieleza sababu za kuzuia maandamano hayo kuwa ni udogo wa barabara za Morogoro na kwamba leo ni siku ya kazi hivyo yanawezesha kusababisha usumbufu kwa wakazi wa mji huo.
Wakati Shilogile akieleza kuzuia maandamano yanayotarajiwa kuanza saa 5 asubuhi, Mkuu wa Operesheni Sangara, Benson Kigaila, alisisitiza kuwa watafanya maandamano kwa kuwa waliskubaliana na Kamanda Shilogile kabla ya kuwageuka.
Kwa mujibu wa Gazeti la Nipashe la 27 August 2012, ilielezwa kuwa Kamanda Shilogile alidai kuruhusu baiskeli na watu kutumia barabara kwa sababu ya mikutano ya Chadema itakuwa ni kuwanyima haki wananchi wengine, na hivyo wataruhusu watu wasiozidi 50 kupita kwa wakati mmoja pasipo kuwa na ishara ya kuonyesha kama wanaelekea katika maandamano.
Ndugu wa marehemu Ally Nzona akiwa amesimama kando ya mwili wa ndugu yake katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro, ambaye alifariki kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamano ya amani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mjini Morogoro
Pichani ni kijana aliyeelezwa kupigwa risasi kichwani katika tafrani hizo na baadae kupoteza maisha Ametambulishwa kwa jina la Ally Zona, ambae alikuwa anasoma magazeti katika stendi ya Msamvu. Tukio hili lilitokea mapema leo asubuhi kuelekea saa sita mchana wakati Polisi walipokuwa wakiwatawanya wafuasi hao wa chadema. Mtoa taarifa anasema Polisi wanadaiwa kutumia risasi za moto pamoja na mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamani hao.
Watu wengine waliojeruhiwa katika tafrani hiyo wameelezwa kuwa ni mwenesha baiskeli Hashim Seif ambae amejeruhiwa kwa risasi mguuni akiwa napita na baiskeli yake na kijana mwingine aliielezwa kuwa ni muuza matunda Frank Valimba ambae amejeruhiwa na risasi tumboni.
Huyu ni mmoja wa majeruhi ambae jina lake halikuweza kupatikana mara moja.
Baadhi ya viongozi wa CHADEMA walikamatwa na kuachiwa kuhusiana na kadhia hiyo ambao ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Hamad Yusuph na Mkuu wa Operesheni Bw Benson Kigaila
Picha za maandamano ni hizi hapa chini
Wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema
Askari waliokuwa katika eneo la tukio kabla ya kuanza kwa maandamano hayo
Moshi wa mabomu yaliolipuliwa kutawanya wafuasi wa CHADEMA
kina mama na watoto wao wakikimbia huku wamezingiriwa na moshi wa mabomu ya kutoa machozi
Mkurugenzi wa Mafunzo wa CHADEMA, Benson Kigaila akionyesha alama ya V wakati akiwa chini ya ulinzi ndani ya gari la Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU)
Wafuasi wa chadema wakiwa na maandamao hayo mjini morogoro
Picha za ziada ni kwa hisani ya Audiface Blog
0 maoni:
Post a Comment