Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MTOTO WA MIAKA 16 APIGWA NA ASKARI POLISI HUKO MANYARA HADI KULAZWA ICU

  • WAMSHAMBULIA KWA MARUNGU NA KUMBANA SEHEMU ZAKE ZA SIRI HADI KUTOKWA NA HAJA NDOGO.

  • APOTEZA FAHAMU NA KULAZWA WODI YA WAGONJWA MAHUTUTI.

JESHI la Polisi Mkoani Manyara limeingia katika shutuma nzito baada ya Askari wake wa tatu kutuhumiwa  kumpiga mtoto mwenye umri wa miaka 16 wa jamii ya kifugaji anayejulikana kwa jina la Kadogoo Kalanga mkazi wa Orkesmet Wilayani Simanjiro hadi kupoteza fahamu.

Tukio hilo lilitokea Jumatatu Agosti 28, 2012  majira ya saa tano na nusu katika eneo la Orkesmet ambapo askari watatu mmoja wao akitambulika kwa jina moja tu la John walimkamata mtoto huyo mara baada ya kumtuhumu kuiba mbuzi wa jirani yake ambaye anajulikana kama Mama Shedi mkazi wa eneo hilo la Orkesmet.

Mashuhuda wanadai kuwa polisi hao baada ya kumkamata mtoto huyo, walianza kumuadhibu bila huruma hali iliyopelekea mtoto huyo kulazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali ya Selian iliyopo jijini Arusha.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa hakuna jarida lolote lililofunguliwa kutokana na kisa hiki. Watu wakaribu na mtoto huyu wanadai kuwa walitaka kufungua mashtaka dhidi ya askari waliofanya unyama huo lakini walikataliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) ndani ya Hospitali ya Selian  mama mzazi  wa kijana huyo, Bi. Paulina Kalanga alisema kwamba askari hao watatu walimfuata kijana wake eneo la mnadani na kumtuhumu kuiba mbuzi na kuanza kumshumbulia kwa kumpiga bila kumpa nafasi ya kujitetea kitendo kilichopelekea kuanza kutokwa na haja ndogo mfululizo na kisha kupoteza fahamu.

“Yaani walimkamata kijana wangu kisha wakaanza kumpiga kwa marungu na mateke ….. wakazishika sehemu zake za siri na kuanza kugongagonga na kitako cha silaha ya moto ndipo alipoanza kujikojolea mfululizo na kupoteza fahamu”alisema huku machozi yakimtiririka

Taarifa zinasema kuwa polisi  hao baada ya kuona hali ya mtoto huyo imekuwa mbaya walimbeba na kisha kumkimkimbiza haraka katika kituo cha afya cha Orkesmet kwa ajili ya matibabu kabla ya wanandugu kuomba gari la wagonjwa mahututi (ambulance) kumkimbiza katika hospitali ya Selian iliyopo mkoani Arusha.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Manyara, Akili Mpwapwa alipohojiwa juu ya tukio hilo alikiri kupata taarifa zake  huku akisema kwa kifupi kwamba tayari ameshatoa maelekezo kwa mkuu wa polisi wilayani humo kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo na kisha aletewe ripoti kamili mezani kwake.

“Nimeshatoa maelekezo kwa OCD kwamba uchunguzi wa kina ufanyike na nipewe ripoti kamili kwa kuwa jana ndiyo nilipigiwa simu na kuelezwa juu ya tukio hilo”alisema

Hatahivyo,aliongeza kwa kusema kwamba endapo kuna askari atabainika kuhusika na tukio hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

“Ikibainika askari amehusika basi hatua kali za kisheria  zitachukuliwa na hapa tayari uchuinguzi unaendelea”alisema

Mtoto aliyepigwa na askari polisi hadi kupoteza fahamu,Kadogoo Kalanga(16)mkazi wa Orkesmet Wilayani Simanjiro akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi(ICU) ndani ya hospitali ya Selian akiwa anahudumiwa na manesi hospitalini hapo juzi jijini ArushA

 

Mmoja wa ndugu wa kijana huyo akiwa anawaonyesha waandishi wa habari ambao hawapo pichani nguo(kaptula) ya kijana aliyepigwa na askari polisi hadi kupoteza fahamu namna ilivyokuwa imechanika chanika baada kushushiwa kipigo

Mama mzazi wa Kadogoo Kalanga ambaye alipigwa na maaskari wa kituo cha Olkesimeti akiwa anaonyesha sehemu ambazo mtoto wake ana maumivu makali baada ya kupigwa!

Wafanyakazi wa Hopsitali ya Seliani wakiwa wanamuhamisha mtoto huyo kwenda Agha Khan  baada ya kukosa kifaa cha kumpima

PUBLISHED BY JAMII BLOG (Pamela Mollel) on 29th August 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO