Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TBL YAZINDUA KINYWAJI KIPYA CHA "MALTIZA" KISICHO NA KILEVI

 

Meneja wa Kinywaji Kipya cha MALTIZA kinachozalishwa na TBL Bi. Consolata Adam akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na kuzinduliwa kwa kinywaji hicho kipya kinachopatikana katika ladha mbili za APPLE na PINE (Pineapple) ambacho amefafanua kwamba Tanzania imekuwa ya kwanza kwa Afrika kuzindua kinywaji cha aina hiyo kisicho na kilevi chenye ubora na kinachotengenezwa na kimea halisi kinachozalishwa hapa nchini.

Bi. Consolata Adam amesema kinywaji hicho kinapatikana katika ujazo wa 330Mls na kimeshasambazwa nchini kote na bei yake ni shilingi 1500, aliongeza kuwa kinywaji hicho ni halisi kisichotiwa rangi na kuwataka Watanzania kujiburudisha na MALTIZA.

Kikundi cha Ngoma kikipamba uzinduzi wa kinywa cha MALTIZA (Deliciously Refreshing),

Sasa kimezinduliwa rasmi.

SKYLIGHT Band na Kikundi cha Sarakasi wakisindikiza uzinduzi huo.

Msanii wa Bongo Flava nchini Mwasiti akitoa burudani huku akisindikizwa na mshehereshaji wakati wa uzinduzi wa kinywaji cha MALTIZA.

Umati wa Wakazi wa jijini Dar uliohudhuria uzinduzi wa Kinywaji Kipya cha MALTIZA ambacho hakina kilevi kinachopatikana katika ladha mbili tofauti APPLE na PINE kinachotengenezwa na kampuni ya TBL uliofanyika Mlimani City jana Augut 25.

Meneja wa Kinywaji Kipya cha MALTIZA kinachozalishwa na TBL Bi. Consolata Adam akiwapa habari njema Wananchi waliohudhuria uzinduzi huo kuwa kinywaji hicho kinafaa kunywewa na Wakubwa kwa wadogo kwa kuwa hakina kilevi, kinaburudisha na kinarejesha nguvu mwilini. Kulia ni Meneja Mauzo wa MALTIZA Bw. Flavian.

PICHA & MAELEZO: DAILY MITKAS BLOG

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO