Wadau wa maji waliofika katika mkutano huo
Mkurugenzi wa AUWSA, Eng.Ruth Koya akiwa anasoma maoni kwa watumiaji maji jana jijini Arusha mkutano ulioshirikisha wadau mbalimbali wa maji
****
Mjumbe wa baraza la watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA(EWURA CCC) Bi..Mayrose Kavura Majinge alisoma maoni ya baraza hilo na kusema katika wasilisho la mamlaka kunamkanganyiko wa taarifa mbalimbali zilizoonyesha kukosekana umakini au upotoshwaji wa maksudi wenye lengo la kuhaalisha maombi ya kupandisha bei ya huduma yamaji
Aidha alibainisha kuwa katika Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu ya Serikali ya mwaka ulioisha June 2011 inaonyesha ufanisi mdogo wa kiutendaji hivyo inaonekana asilimia kubwa ya watumiaji wa maji hawalipi huduma hiyo hivyo kupandisha bei kutamuumiza mwananchi
Akifungua Taftishi hiyo mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela kwa niaba ya RC wa mkoa huu alisema kuwa
Watumiaji,wadau wa huduma ya maji wanao wajibu wa kulipia huduma ya maji kwani haki bila wajibu ni vurugu,na wajibu bila haki ni utumwa hivyo wanao wajibu wa kulipia huduma hizo kikamilifu na kwa wakati
Bw.Mongela alisema kuwa AUWSA wanawajibu pia wa kuwapa huduma iliyosahihi watumiaji wahuduma hiyo na kuacha kutumia njia hiyo kuwakandamiza wananchi kwani kukosa huduma kwa mwezi halafu unalipia huo utakuwa ni wizi na kuwarudisha nyuma wananchi.
Naye mkazi wa jijini hapa Bw. Alli Iddy akichangia hoja, aliwataka AUWSA kutafuta wawekezaji wa maji ili tatizo la uhaba wa maji hapa Mkoani lipatiwe ufumbuzi zaidi ya kupandisha bei ya maji
SOURCE: JAMII BLOG “Pmela Mollel”
0 maoni:
Post a Comment