Mwenyekiti wa Umoja wa Walimu nchini Kenya (KNUT) Wilson Sossion akizungumza katika mkutano wao wa kujadili hatua mbambali za mgomo wao unaotaraji kuanza wiki ijayo nchini kote. KNUT walikutana Agosti 29, 2012 mjini Nairobi.
Umoja wa Walimu nchini Kenya (KNUT) kimekutana leo jumatano mjini Nairobi kujadili hatua za mgomo unatarajiwa kuanza wiki ijayo.
Mwenyekiti wa KNUT , Wilson Sossion (pichani) alisema mkutano huo ni wa kurasimisha mgomo na kupanga shughuli ambazo walimu watakuwa wakifanya katika wakati huo wa mgomo.
"Hadi sasa, hakuna kiongozi yeyote wa serikali amesema lolote juu ya mgomo huu, hivyo basi mamlaka yetu kuendelea na wito juu ya kuwapo kwa mgomo," alisema.
Aidha katika mkutano huo wa jana Jumatano, alibainisha, utawaleta pamoja wanachama 440 wa Kamati ya kitaifa ya ushauri ambayo itaidhinisha mgomo pindi watakapo kutana katika Kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta mjini Nairobi.
“Zaidi ya uamuzi wa kamati ya ushauri, baraza la taifa la utendaji litakutana na kusimamia utekelezaji wa mgomo," Sossion aliongeza.
KNUT ilikuwa imetoa ilani ya siku saba kwa serikali tangu Agosti 19 na kueleza kuanza rasmi kwa mgomo ni Septemba 3, wakati shule zikiwa zimefunguliwa.
Tayari serikali, Wizara ya Elimu pamoja na Tume ya huduma kwa Walimu Wamejiweka mbali na madai ya KNUT.
KNUT inadai nyongeza za mishahara na posho nyingine ya jumla ya zaidi ya Sh43 bilioni za Kenya, sehemu ambayo ilifikiwa maamuzi 1997 wakati wa utawala wa Rais Moi na kiasi fulani ulianza kutekelezwa.
Hii ni pamoja na kiasi cha asilimia 300 ya nyongeza ya mshahara, pamoja posho uwajibikaji asilimia 50, asilimia 40 na asilimia 30 kwa ajili ya walimu wakuu na manaibu wao pamoja na walimu waandamizi na wakuu wa idara.
Source: http://mrokim.blogspot.com
0 maoni:
Post a Comment