Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: MKUTANO WA GODBLESS LEMA NA JAMES MILLYA ARUMERU MAGHARIBI JANA

DSC05212

James Ole Millya, kamanda mpya wa CHADEMA akizungumza na wananchi (hawaonekani pichani) wa Kata ya Bang’ata iliyopo Jimbo la Arumeru Magharibi jana katika mfululizo wa operasheni za kuimarisha chama hicho maeneo tofauti ya nchi. Millya aliambatana na aliekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Mh Lema ambe rufaa yake ya kupinga kuenguliwa ubunge wake itasikilizwa Septemba 20 mwaka huu.

Katika msafara huo, walikuwako pia makamanda wengine kutoka Arusha na ‘kamanda’ Christopher Mbajo ambae amewahi kuripotiwa kuwakosesha amani Waziri wa Kilimo Mathayo David na Mama Anne Kilango katika majimbo ya Same kupitia mikutano aliyoshiriki jimboni humo ili kuimarisha chama nyumbani kwake mkoani Kilimanjaro.

DSC05113Nuru Ndosi (juu ya meza kulia) ambae ni Katibu wa chama hicho Kata ya Nkoanrua Jimbo la Arumeru Mashariki akizungumza na wananchi hao

DSC05179

DSC05214Mh Lema kifafanua maswala mbalimbali katika mkutano huo

DSC05165James Ole Millya (mwenye skafu) katika benchi la viongozi na makamanda waalikwa katika mkutano huo

DSC05184

DSC05220Kina mama waliokabidhisha kadi za CCM wakisubiri kupatiwa kadi mpya za CHADEMA kutoka kwa Lema ambe aliwalipia gharama za kadi hizo wote.

DSC05223Hapa Mh Lema akiandikisha na kusaini kadi za wananchama hao wapya huku Millya kitazama pembeni. Pia wananchi wengine ambao hawakuwahi kuwa wanachama wa chama chochote nao walinunua kadi za CHADEMA kwa wingi  hadi kkumalizika furushi walilikwenda nalo kama picha ya chini inavyoonesha.

DSC05229

Lema akishauriana jambo na Christopher Mbajo (mwenye shati ya bluu), kada mwingine wa chama hicho marufu kutoka Same, ili kuona namna ya kufanya baada ya kadi kuwaishia na watu bado walikuwa wanahitaji. Katika hotuba yake alipopewa nafasi ya kuzungumza, Mbajo aliwaasa wananchi hao kutohadaika na propaganda za CCM zinazolenga kukichafua CHADEMA na kuwataka kuiunga mkono CHADEMA katika harakati zake za kumpigania mtanzania kwa madai kwamba ndio chama pekee ambacho kimeweza kuonesha na kina dhamira ya kweli kuwapigania wanyonge wa taifa hili. Picha zote na Nuru Ndosi.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO