Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA) Mh Joseph Mbilinyi almaarufu Sugu ambae bado yuko nchini Marekani na Mwenyekiti wa chama chake taifa Mh Freeman Mbowe kwa shughuli za chama anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye tukio lingine la cham hicho kama tangazo hili linavyoeleza.
Kwa mujibu wa maelezo ya Sugu kupitia akaunti yake ya Facebook amewashukuru wanaCHADEMA waishio Houston Texas Marekani kwa kujitolea pikipiki 126 kwa ajili ya kusaidia kusambaza harakati za CHADEMA kama sehemu ya ushiriki wao kuiondoa CCM madarakani ifikapo Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Uzinduzi wa tawi la Houston Texas
Juzi tarehe 25 August 2012 jijini Houston, Texas nchini Marekani Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kilifungua tawi lingine la pili tarehe baada ya kufungua tawi la awali Jijini Washington DC tarehe 27 MAY 2012, ikiwa ni muendelezo wa kufungua matawi mbalimbali nchini humo.
Sherehe hiyo ya Ufunguzi wa Tawi la Chadema Houston imehudhuriwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe Freeman Mbowe na Mbunge wa Mbeya mjini Mhe Joseph Mbilinyi "Sugu".
Viongozi wengine waliohudhuria ni Katibu wa Chadema Tawi la Washington DC Mhe Isidory Lyamuya na aliyekuwa katibu wa Kwanza wa Chadema Washington DC Mhe Liberatus Mwang'ombe.
Sherehe hizo ambazo zilifanyika katika Hotel ya Marriot zilihudhuriwa na Watanzania wengi waishio Houston. Katika Sherehe hizo wanachama wengi waliamua kujivua gamba na kuvaa Gwanda kama ishara ya kutaka kulikomboa Taifa la Tanzania linalozama katika Bahari ya Mafisadi.
Akiongea katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chadema Houston Ndugu Fuefue ameahidi kufanya mambo makubwa kwa kushirikiana na wanachadema wa Houston na wapenda mabadiliko wote kuchangia kwa hali na mali katika operesheni inayoendelea hivi sasa ya M4C. Viongozi hao wa Chadema Houston wameahidi kuchangishana pesa ili kununua gari litakalosaidia katika operesheni ya M4C, pamoja na ahadi ya kutoa pikipiki 116 kama mchango wao kwa Chama kwa ajili ya M4C.
0 maoni:
Post a Comment