Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Machinga waandamana jijini Arusha

Zaidi ya wamachinga 600 jana waliandamana mpaka ofisi ya meya jijini Arusha kupinga tamko la kuwataka wahame katika maeneo ya mjini kwa kile kilichodaiwa kuwa  sio sehemu zao za biashara na kukaa huko wanafanya mji uwe mchafu

Wakizungumza wakiwa nje ya ofisi ya Meya wa jiji la Arusha wamachinga hao walisema kuwa wamekuja kulalamikia uamuzi uliotolewa na manispaa ya jiji  kuwa wanawataka wahame katika maeneo hayo ya katikati ya jiji.

Mmoja wa wawamachinga alisema kuwa aliyejitambulisha kwa jina la Hatibu Hamisi alisema kuwa wao ni wafanyabishara ambao walitegemea kuwa kupatia kipato kwani ni sehemu ambayo wananchi wangi wanapita na kuna wateja wengi lakini huko ambapo wanawapeleka hawatapata wateja kwani hamna mzungumko mkubwa wa wateja.

Alisema kuwa wanaomba wafikiriwe kwani wao kama wamachinga wanategemea kupata kipato kutoka kwa wananchi wanaopita  huku wengine wakitegemea wageni.

Gazeti lilimtafuta meya wa jiji la Arusha Gaudence Lyimo ili azungumzie sakata hilo la maandamano hakuweza kupatikana ofisini kwake ndipolilipowakuta baadhi ya madiwani wakijadili swala hili .

Akiongea kwa niamba ya meya wa jiji la Arusha Ishmaeli katamboi naye alisema kuwa wamelipata tatizo hili bali maneo ambayo wanayalalakia sio ya kwao bali ni ya halmashaur ya jiji huku akibainisha kuwa hamda eneo lolote lililopo katika halimashauri  ni  la mtu bali maeneo hayo yapo kwa mujibu wa sheria.

Alisema kwamba wamekuwa wakifanya biashara kinyume cha sheria pembezoni mwa barabara na mbele ya maduka ya wanyabishara wakubwa na kusabisha msongamano wa magari na wengine kupanga vitu pembezoni mwa barabara hali inayofanya waendo kwa miguu kupata adha wakati wakitoka sehemu moja kwenda ingine.

Machinga ndani ya zanzibarMachinga wa nguo mjini Zanzibar (Picha ya maktaba kwa hisani ya Ommi Kiss wa Zanzibar)

Alisema kuwa mwanzoni mwa mwezi huu walikaa na vingozi wao na kubaini sehemu za kuwapeleka wafanya biashara hao ambao ni wamachinga kwa muda hadi pale watakapo pata maheneo mengine ya kufanyia biashara na pia wap kwenye mpango wa kuandaa maeneo ambayo yatakuwa yakudumu.

Alitaja maeneo ambayo yametengwa kwa muda kuwa ni Samunge A na B ambapo alisema kuwa maeneo haya yapo katika kata ya levolosi karibu na soko la kilombero ,hata ivyo manispaa wameona watumie busara na hekima ya kuwatafutia maeneo hayo kwani walikuwa na uwezo wa kuwatoa kwa kufuata sheria huku akibainisha kuwa zoezi hilo halitaishia hapo bali ni endelevu.

Katamboi alisema kuwa kuna baadhi ya wafabiashara ambao teyari wanasehemu yakufanyia bishara ambayo walipatiwa na halmashauri lakini na wao pia wanaandamana ili wapate sehemu ingine ambapo alisema kuwa wao kama viongozi na madiwani hawatakuwa tayari kuwapatia viwanja mara mbili.

"nia ya kufanya haya yote  ni pamoja na kutaka kuliweka jiji letu katika usafi na muonekano wenye hadhi ya jiji la kitalii na napenda kuwaomba wananchi wote kwa ujumla kutoa ushirikiano katika kufanikisha zoezi hili na kuanzia sasa tumeweka sheria ambayo mtu yeyote atake onekana ametupa uchafu ama ametema mate atalipa faini au kifungo au vyote kwa pamoja"alisema Katamboi

Alibanisha kuwa jiji likiwa safi litatuletea faida kwani wageni wengi na wafanyabiashara wakubwa wakiwemo wawekezaji watavutika kuja kwani ni maeneo salama kwa biashara zao na pia uchumi utapanda kulingana na ugeni huo.,

Sourced from: mdau Father Kidevu

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO