Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Polisi kufunguka leo kuhusu kilichomkuta Dk Ulimboka

POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, leo watazungumzia hatua ilizofikia katika uchunguzi wa tukio la kutekwa, kuteswa na kutupwa katika Msitu wa Pande kwa kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk Steven Ulimboka.

Pamoja na suala la Dk Ulimboka, imesema pia itazungumzia mambo kadhaa yanayohusu usalama wa nchi.
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova aliliambia gazeti hili kuwa atazungumzia suala la Dk Ulimboka ili kuweka wazi kwa umma kuhusu tukio hilo lililokuwa gumzo katika siku za hivi karibuni.

Kamanda Kova alitoa kauli hiyo alipotakiwa na gazeti hili kueleza endapo Dk Ulimboka ni mmoja wa mashahidi katika kesi iliyokwishafunguliwa kuhusu tukio la kutekwa kwake.

“Tutazungumza na wananchi na wanahabari kwa ujumla kuhusu mambo mengine yanayohusu usalama wa nchi pamoja na hatua tulizofikia katika uchunguzi wa kitendo cha kutekwa na kupigwa kwa Dk Ulimboka,” alisema Kova.

Hata hivyo, Kova hakutaka kuzungumzia suala la mtu anayedaiwa kujitokeza na kukiri kuwa ndiye mtekaji wa Dk Ulimboka na yale yaliyoandikwa katika gazeti la Mwanahalisi akidai kuwa mambo hayo yapo mahakamani.

“Sisi tutaweka wazi wajibu tulioufanya na hatua tulizofikia kuhusu kutekwa kwake, mambo mengine ni ya kimahakama, hatuwezi kuyaingilia,” alisema Kova.

Kova aliwataka Watanzania kuliamini Jeshi la Polisi na kusisitiza kuwa linafanya kazi yake kwa uadilifu na litahakikisha kuwa ukweli kuhusu tukio hilo lililovuta hisia za watu wengi, unafahamika.
Source: Mwananchi

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO