Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CHADEMA Arusha yavuna wasanii 41

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoa wa Arusha, Mwigamba Samson amewapokea wanachama zaidi ya 40 ambao ni wasanii wa kikundi cha Serengeti Art Group kama wanachama wapya wa chama hicho katika halfa iliyofanyika katika ofisi za chama hicho Mkoani na kuhudhuriwa na viongozi wengine ngazi ya Mkoa wakiwemo Mwenyekiti wa Vijana, Ephata Nayaro na Katibu wa chama Mkoa, Amani Golugwa.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa inashangaza kuona wasanii wengi wa Tanzania wana hali mbaya kiuchumi licha ya kazi kubwa na nzuri wanazozifanya na kuongeza kuwa hali hiyo inasababibshwa na serikali iliyopo madarakani kutojali kazi hizo. Amesema kama chama na kupitia wabunge wa chadema wamefanya kazi kubwa ya kuishinikiza serikali kuliona hilo na kulifanyia kazi.

Kwa upande wake Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha Amani Golugwa, amesema sera ya chama chake kuhusu sanaa ni kuona kuwa sanaa haibakii kutumbuiza peke yake bali ni kuhakikisha kuwa inakua ajira rasmi kwa wasanii na wadau wanaojihusisha nayo kwa namna moja ama nyingine.

Katibu huyo ameongeza kuwa vuguvugu la mabadiliko linaloendelea hivi sasa lina lengo la kuzidi kukiimarisha chama na kwamba mkoani Arusha vuguvugu hilo litafanyika mnamo mwezi wa kumi na moja hivyo amewataka wanacham hao wapya kuanza kazi ya kuleta mabadiliko kama lengo la vuguvugu hilo linavyosema.

Mwnyekiti wa kikundi cha Serengeti akikabidhiwa katiba na kadi ya uanachama ya CHADEMA na Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Arusha, Samson mwigamba huku Katibu wake Amani Golugwa na Mwenyekiti wa Vijana Mkoa, Ephata Nayaro (mwenye shati jeupe) wakishuhudia. Picha chini zinaonyesha baadhi ya wanakikundi hicho wakipokea kadi mpya za uanachama.


Baadhi ya wasanii hao ambao wamevua gamba na kujiunga rasmi na chadema

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO